Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, June 24, 2018

Godbless Lema Aguswa Na Hali za Vigogo wa Escrow Wanaosota Mahabusu

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwaone huruma watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi, wafanyabiashara Harbinder Seth  pamoja na James Rugemalila kwa kuitaka serikali ikamilishe upelelezi kwani watu hao wanapitia mateso kwa kukaa mahabusu.

Lema ameonyesha kuguswa na watu hao baada ya picha zao kusambaa siku ya Jumatano hii walipokuwa wamekwenda kusikiliza kesi yao huku upande wa mashtaka wakidai kuwa bado upelelezi haujakamilika.

"Ninaona huruma juu yenu. Serikali kamilisheni upelelezi juu ya watu hawa kama wanastahili adhabu walipe walichopanda, kuwa mahabusu bila kesi yako kusikilizwa ni mateso kuliko mnavyoweza kufikiri".

Ameongeza Pengine wanastahili adhabu lakini ni vyema Mahakama ifanye maamuzi.

Seth na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi.

Pia, wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22 milioni za Marekani na Sh309.46 bilioni
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...