Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, June 20, 2018

Hukumu ya Wema Sepetu ni July 16

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu  inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili July 16,2018.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mawakili wa upande wa utetezi kufunga ushahidi wao wa mashahidi watatu akiwemo Wema.

Mbali ya Wema, katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abas.

Hakimu Simba amesema mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo July 16,2018 baada ya kufungwa kwa ushahidi wa utetezi uliokuwa na mashahidi 3 akiwemo Wema.

Awali kabla ya kupangwa kwa tarehe ya hukumu Wema na wafanyakazi wake walijitetea, ambapo Wema amedai kuwa ni kweli nyumbani kwake kulikutwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi na vipisi.

Katika hoja zake, Wema amedai kuwa hajui vitu hivyo ni vya nani kwa sababu yeye ni msanii wa Filamu na nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya Party na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mchana.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )