Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 9, 2018

Mameneja Masoko Sita Manispaa Ya Ubungo Watumbuliwa KwA Ubadhirifu wa Milioni 293

adv1
Kamati ya fedha ya Manispaa Ubungo jijini Dar es Salaam, imemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwasimamisha kazi mameneja wa masoko sita na watumishi watatu kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha Sh milioni 293.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Juni 8, Meya wa Manispaa hiyo, Boniface Jacob, alisema hatua hiyo ni kutoka na ripoti ya Mkaguzi wa Manispaa ya uchunguzi wa ukusanyaji wa mapato katika  masoko 16 ya wilaya hiyo.

Aliwataja wanaotakiwa kusimamishwa na na masoko yao kwenye mabano kuwa ni Obote Etta (Soko la Ndizi Mabibo),  Grayson Sebastian (Simu  2000), Frida Michael (Shekilango), Edwin Mugila (Mabibo) na Bakari Mshanga (Sinza) kwa upande wa watumishi wa Manispaa ni Mweka Hazina, Ofisa Mapato na Msimamizi wa Mfumo.

“Baada kutoridhishwa na taarifa ya mapato yatokanayo na masoko, Mkaguzi wa Manispaa ilibidi akachunguze kilichosababisha makusanyo kushuka hadi milioni 716.

“Ripoti yake imebaini ubadhirifu wa zaidi Sh milioni 293 ambapo mapato halali yanayoonekana kwenye mfumo ni zaidi ya Sh bilioni moja lakini baada ya kuwabana wamerejesha kiasi cha Sh milioni 139,” alisema Jacob.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )