Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 21, 2018

Mbunge CCM Aipinga Serikali Kununua Ndege Badala ya Kuboresha Huduma za Afya, Barabara

Mbunge wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu amesema ununuzi wa ndege za Bombardier uliofanywa na Serikali hauna tija kwa wananchi wa jimbo lake iwapo huduma za afya na barabara hazijaboreshwa.

Kadutu ametoa kauli hiyo jana Jumatano Juni 20, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma.

Alisema umebaki mwaka mmoja kabla ya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hivyo ahadi zilizotolewa zinapaswa kutekelezwa.

“Serikali imejenga reli, inanunua ndege hebu twendeni kwa wananchi, ujue ukienda kule Ulyankulu ukauliza Bombardier hawakuelwi, barabara mbovu, afya mbovu hawakuelewi,” alisema Kadutu.

“Pelekeni fedha barabara ziboreshwe, Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini) wapewe fedha. Bajeti iliyobaki ni moja ya kujadili kwa utulivu kwani akili itakuwa majimboni tu, tusaidieni ili mwaka 2020 tupete,” alisema.

Akigusia  ahadi za kampeni za uchaguzi, Kadutu alisema waliahidiwa jimbo la Ulyankulu litakuwa wilaya lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

“Hamtaki kutupa eneo lakini mnasema ahadi za Rais zitatekelezwa, sasa hii ni ahadi ya Rais, alisema akiingia siku tatu tu tunapata wilaya,” alisema.

“Sasa imebaki mwaka mmoja tu na nusu yako mengi, mmetuahidi lami tena kilomita tatu tu lakini tunaona mambo ambayo hayako katika ilani yanatekelezwa. Tukisema…,mimi watu wa Ulyankulu wamenituma.”

Mbunge huyo amesema anashangazwa na mawaziri kutotembelea jimboni kwake huku wakionekana kupishana katika majimbo mengine jambo linalokatisha tamaa wananchi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )