Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 19, 2018

Misri Yatandikwa Tena Bao 3-1 na Urusi....Kwa Matokeo Haya, Misri ndo Basi Tena!!

Timu ya taifa ya Misri huenda ikawa timu ya kwanza kuaga Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo pamoja na kuwa kimahesabu inaweza kuwa bado, lakini kiuhalisia ni ngumu.

Misri ambayo ilifungwa bao 1-0 na Uruguay kwenye mechi yake ya kwanza, leo tena imekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wenyeji Urusi hivyo kuwa na hali mbaya katika Kundi A.

Msimamo wa Kundi A lenye timu za Urusi, Saudi Arabia, Misri na Uruguay unaongozwa na wenyeji Urusi wenye alama 6 kwenye mechi mbili wakifuatiwa na Uruguay yenye alama 3 kwenye mechi 1.

Saudi Arabia zinavutana na Misri mkiani ambapo Saudi Arabia imepoteza mechi moja dhidi ya Urusi ilipofungwa mabao 5-0 kwenye mechi ya ufunguzi.

Misri ili isonge mbele inahitaji kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Saudi Arabia kwa kuanzia mabao angalau 5 kwenda juu huku ikiomba Uruguay ipoteze dhidi ya Saudi Arabia kwa idadi ndogo ya mabao. Kiujumla Misri imeaga michuano.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )