Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, June 24, 2018

Mnyeti Afungua Kiwanda Kilichofungwa na Mkea Mkuu wa Serikali, Ataka Akamatwe Yeye Badala ya Mmiliki

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amekifungua kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brand cha mjini Babati kilichofungwa na Mkemia Mkuu wa Serikali huku akitaka akamatwe yeye, badala ya wamiliki wa kiwanda hicho.

Mnyeti ameyasema hayo juzi wakati akichukua uamuzi huo ambapo amefafanua kwamba hakubaliani na sababu zilizotolewa mpaka kiwanda hicho kufungwa

Akitoa maelezo Mnyeti amesema mwekezaji huyo amefunga mitambo yake na kutoa ajira kwa wananchi, badala ya kupewa ushirikiano watendaji wanaohusika, wao ndiyo  wanamkwamisha kwa kukifunga kiwanda, ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa.

"Bado kuna watu wanaandaa mazingira ya rushwa, yaani badala watumie hata siku tatu za kumshauri kitaalamu wanakimbilia kufunga kiwanda. Kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wana ukiritimba mno, sasa mimi nakifungua kiwanda hiki halafu wakija wanikamate mimi," alisema.

Mkemia Mkuu wa Serikali alikifunga kiwanda hicho kwa maelezo kuwa kimekosa kibali cha kuidhinisha matumizi ya kemikali za kuzalisha pombe hizo Machi, 2018
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )