Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, June 21, 2018

Shamsa Ford Amkingia Kifua Irene Uwoya Baada Ya Picha Yake Ya Nusu Uchi Kusambaa

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kumkingia kifua Msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake ya utata kusambaa mtandaoni.

Siku ya jana Irene Uwoya alitengeneza headlines baada ya kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha maungo yake nje ndani ya nguo ya kuogelea.

Watu walimjia juu Uwoya baada ya picha ile kusambaa ingawa mwenyewe alijitetea kuwa alikuwa yuko Beach na lile ni vazi la kuogelea hivyo haoni tatizo.

Shamsa amemtetea Uwoya na kuweka wazi kuwa haoni kama kuna kosa yeye kuvaaa vile hasa ukiangalia alikua mazingira ya baharini hivyo kuvaa vazi la baharini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa aliandika ujumbe huu:

"Picture zako zote nzuri mama umependeza sana, mimi nachojua mtu unavaa kutokana na location unayoenda, sasa sidhani kama Ir.Kuna wengine wanavaa en anaweza akavaa hivi halafu akaenda ofisini. Sasa mtu yupo beach mlitaka avae dira.

"Mumewe amemsifia amependeza sasa nyie wapembeni mnasema amekosea mnajisumbua, kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake binafsi na Mungu. Tusiishi kwa kuhukumiana maana wa peponi hawajulikani.

"Hadi dira beach lakini matendo yake ukiyashuhudia unaweza ukatoa mbio. Tatizo lako wewe dada Iren ni hilo umbo ndo limewakosesha amani watu.Ungekuwa na flatscreen maneno yasingewatoka hebu kafanye operation upunguze Gushepu“.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )