Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 5, 2018

Simba Yatinga Nusu Fainali Sportpesa Super Cup Nchini Kenya

Mabingwa  wa Tanzania Bara, Simba SC jana  wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Kariobangi Sharks kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Shujaa wa Simba SC jana  alikuwa ni kipa wake hodari, Aishi Salum Manula aliyeokoa penalti na sasa Wekundu hao wa Msimbazi watakutana na mshindi wa mchezo wa leo  kati ya wenyeji wengine, AFC Leopards dhidi ya Singida United kwenye Nusu Fainali.

Waliofunga penalti za Simba SC ni Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni na Jonas Mkude, wakati Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Paul Bukaba walikosa.
 
Simba SC pia imeifutia aibu Tanzania baada ya juzi  Yanga SC na JKU ya Zanzibar kutolewa na  timu za Kenya katika hatua ya kwanza tu ya michuano hiyo.
 
Ilianza Yanga SC kuchapwa 3-1 na Kakamega Homeboyz hapo hapo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Allan Watende Wanga akifunga mabao mawili dakika za 26 na 30 na linguine la Kakamega Homeboyz likifungwa Wycliffe Opondo dakika ya 85, huku la timu ya Jangwani mjini Dar es Salaam likifungwa na Matheo Anthony dakika ya 38.

JKU nayo ikafuatia baada ya kuchapwa 3-0 na mabingwa watetezi, Gor Mahia mabao ya George Odhiambo, Godfrey Walusimbi na Meddie Kagere.

Kakamega Homeboys sasa watakutana na Gor Mahia katika Nusu Fainali Juni 7, na Nusu Fainali ya pili itaikutanisha Simba SC na washindi wa mechi za leo
 
Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
 
Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )