Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 25, 2018

TRCRA Kushirikiana na Polisi Kuwakabili Wezi wa Njia ya Mitandao

Serikali imesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Polisi watahakikisha wanafanya kazi kwa ukaribu kuhakikisha wote wanaotapeli kwa njia ya mitandao wanakamatwa na kuchukuliwa hatua  kali za kisheria.

Hayo yamebainishwa  kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Bungeni Jijini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali aliyehoji; “Kumekuwa na wimbi sasa limeibuka la wizi wa kutumia mitandao ya simu wakiwa wanatuma sms kuwa umeshinda ‘Tatu Mzuka’ mara umeshinda Tigo, tuma pesa kwenye namba hii,kumekuwa na desturi hiyo sasa hivi. Nilitaka kupata majibu kutoka kwa Waziri TCRA imechukua juhudi gani wizi wa kutumia simu kwenye mitandao unakomeshwa na kuhakikisha wahusika wanakamatwa?

“Ni kweli kwamba kumekuwa na matukio ya kutumiwa sms Watanzania mbalimbali ambazo zinaonyesha viashiria kwamba kuna utapeli unaoendelea katika huduma za mawasilino lakini kwa kutumia sheria ya 2015 ya wizi wa mitandao TCRA kwa kushirikiana na Polisi wameendelea kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha kwamba wote wanaosambaza ujumbe huo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,” amesema Nditiye.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )