Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 23, 2018

Trump asema Korea kaskazini bado ni 'tishio kubwa'

adv1
Rais wa Marekani Donald Trump ameidhinisha upya vikwazo dhidi ya Korea kaskazini akitaja taifa hilo kuwa 'tishio lisilo la kawaida' kutokana na silaha zake za nyuklia - siku 10 tu baada ya kutamka kwamba hakuna hatari yoyote kutoka kwa Pyongyang.

"Hakuna tena tishio kutoka Korea kaskazini," alituma ujumbe mnamo Juni 13, siku moja baada ya kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un huko Singapore.

Hatua hiyo imekuja wakati Marekani na Korea kusini zimefutilia mbali mazoezi mawili ya pamoja ya kijeshi.Wizara ya ulinzi Marekani Pentagon imesema lengo ni kuunga mkono majadiliano ya kidiplomasia.

Marekani imekuwa na 'hali ya dharura kitaifa' iliyoidhinishwa kuhusiana na Korea kaskazini tangu 2008.

Tangu hapo marais wamekuwa wakiidhinisha hali hiyo kuendelea mtawalia na vikwazo dhidi ya Pyongyang.

Rais Trump aliendeleza hali hiyo ya dharura jana Ijumaa kutokana na 'uwepo wa hatari ya kuongezeka kwa silaha katika rasi ya Korea na hatua na sera za serikali ya Korea kaskazini'.
 
Haya "yanaendelea kuzusha tishio lisilo la kawaida kwa usalama wa kitaifa, sera ya nchi za nje na uchumi wa Marekani", alisema katika taarifa kwa bunge.

Wanachama wa Democratic wanasema tamko la sasa kutoka ikulu ya White House linakwenda kinyume na majigambo ya awali ya rais Trump kuhusu ufanisi wa mkutano wa Singapore.
 
Katika mkutano huo wa kihistoria kati ya rais wa sasa wa Marekani na kiongozi wa Korea kaskazini Viongozi hao walisaini taarifa ambapo Marekani iliahidi usalama kwa Korea kaskazini na mwenzake akaahidi "kushughulika kusitisha mipango ya nyuklia katika rasi ya Korea" - pasi kufafanua maana ya ndani ya makubaliano hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kuwa vikwazo dhidi ya Korea kaskazini vitasalia wakati majadiliano yanaendelea kuhusu silaha zake za nyuklia.

Hatahivyo, vyombo vya habari Korea kaskazini vimeripoti kuwa Trump alikubali 'kuondosha vikwazo' wakati uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ukiendelea.

Credit:BBC
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )