Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 12, 2018

Wachina 19 na Watanzania 6 wafikishwa Mahakamani kwa uhujumu uchumi

Raia 19 wa China na Watanzania 6, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao wanashtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya uhamiaji, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania na uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao ni Bo Song, Liu Yunley, Chen Chao Hui, Fu Zeng, Wu Hai Quing, Ke Qiu Fang, Frederick Kumalija, Jing Jing Lin, Ku Liao, Yan Yan Geng, Chen Ying Gong.

Salim Mahsein Al-Amry, George Elikana, Fatuma Songoro, Bhoke Mwita, Kelvin Ponela, Chen Gwandi, Lin Ben, Rui Guo, Lin Xiangqui, Chen Fa, Wan Li, Robert Mkini na Revocatus Mugisha.

Akiwasomea mashtaka yao Wakili wa Serikali Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amedai kuwa June Mosi 2017 na May 18/2018 wanadaiwa walitoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata kibali cha kufanya kazi nchini.

Pia wanadaiwa siku na mahali hapo hapo, washtakiwa wote wa makusudi walitoa taarifa za uongo kwa Kamishna wa kazi kwa lengo la kupata vibali vya kufanyia kazi.

Katika shtaka la Tatu, mshtakiwa Bo Song anadaiwa kuijihusisha na kazi nchini bila ya kuwa na hati ya kuishi nchini.

Katika shtaka la nne, washtakiwa ni Kumalija, Mwita, Songoro, Ponela, Mkini na Mugusha ambapo wanadaiwa kuwa kati ya June Mosi 2017 na May 17/2018 ndani ya Jiji la Dar es Salaam, walimsaidia raia wa China, Bo Song kujihusisha na kazi nchini huku wakijua kuwa hana kibali cha kuishi nchini wala kufanya kazi.

Katika shtaka la tano, washtakiwa wote wanadaiwa kuandaa, kusimamia na kusaidia kutoa taarifa za uongo kwa dhumuni la kujipatia kibali cha kufanya kazi na kuishi nchini.

Shtaka la mwisho, washtakiwa wote kinyume na sheria ya uhujumu uchumi, walijihusisha na makosa ya kiudanganyifu kwa kuonyesha kwamba walikuwa na vibali vya kuishi nchini Tanzania kutoka idara ya Uhamiaji na vibali vya kufanya kazi kutoka kwa Kamishna wa kazi nchini huku wakijua kuwa siyo kweli

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Pia DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi ya washtakiwa kwa ajili ya maslahi ya nchi na washtakiwa. Hata hivyo upande wa utetezi kupitia Peter Kibatala umepinga zuio hilo la dhamana.

Baada ya mabishano ya kisheria, Hakimu Shaidi amesema atatoa uamuzi dhidi ya washtakiwa kama wapate dhamana ama la June 14, 2018
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )