Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, June 12, 2018

Wanafunzi wa UDSM kuzikwa Ijumaa

Taarifa kutoka uongozi wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), zinasema miili ya waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho Steven Sengo na Maria Soko wanatarajiwa kuzikwa Ijumaa Juni 15, 2018, Jijini Dar es Salaam.
 
Katibu Mteule serikali ya wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu Dar es Salaam, Hussein Amri Aman amesema kuwa ndugu wa marehemu Steven Sengo wamepanga azikwe siku ya Ijumaa Juni 15, 2018 na kuongeza kuwa kwa sasa uongozi huo unafanya utaratibu wa kuchangisha rambirambi.

“Sasa hivi kinachoendelea tunakusanya rambirambi kwa wanafunzi na taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu Bwana Steven Sengo zinasema kwamba wao watafanya mazishi siku ya Ijumaa na mazishi yatafanyika Yombo Vituka” amesema Bwana Aman.

Aman ameongeza kuwa uongozi wa wanafunzi umewasiliana na ndugu wa marehemu Maria Soko aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na kubainisha kuwa nae atazikwa siku ya ijumaa Juni 15, 2018 maeneo ya Boko-Bunju Jijini Dar es salaam.

Katibu huyo amesema kuwa Serikali ya wanafunzi inaongea uongozi wa Chuo ili kuandaa utaratibu wa kuwezesha miili ya marehemu wote kuugwa na wanafunzi wenzao Chuoni hapo kabla ya kupelekewa kwa ndugu kwaajili ya mazishi.

Mpaka kufikia sasa wanafunzi wawili na watumishi wawili wa chuo hicho wamefariki Dunia baada ya gari la wagonjwa waliokuwa wamepanda kugongana na lori la mizigo katika eneo la Riverside usiku wa Jumatatu Juni 11, 2018. Majina ya marehemu ni Maria Soko, Steven Sango, dereva aliyejulikana kwa jina la james na muuguzi Jonathan Lugando (40)
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )