Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Bodi Ya Nyama Nchini Yaanza kuwabana Vishoka Wanaowauzia Wateja Nyama Za Punda, Mbwa Bila Ridhaa Yao

Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Bodi ya Nyama Tanzania imeanzisha utaratibu wa kuwasajiri wafanyabiashara wa Nyama wakiwemo wachinjaji kwa lengo la kudhibiti vishoka wanaouza Nyama haramu kinyume cha sheria
 
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof,Faustine Lekule ameyasema hayo jijini Arusha katika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Nyama nchini baada ya kutembelea viwanda vya Nyama ,Wafugaji na wachinjaji na kujionea changamoto zinazowakabili.
 
Amesema mpango huo utasaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa walaji kutokana na baadhi ya wauzaji wa nyama kutokuwa waaminifu kwa kuwachangajia Nyama zisizostahili ikiwemo za wanyama  Punda,Mbwa,Paka bila ridhaa ya Mlaji.
 
Pia amesema bodi yao imelenga  kuwaunganisha wachinjaji wa Nyama ,wafanyabiashara wa Nyama na masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi, na kuwataka wachinjaji  wahakikishe wanauza Nyama yenye ubora unaostahili.
 
Amesema bodi hiyo kupitia ofisi zake zilizopo wilayani itasajiri wachinjaji wa Nyama na kuwapatia vibali maalumu ili kupunguza vishoka kufanyabiashara hiyo kinyume na uaratibu
 
“Suala  la uchinjaji na uuzaji wa Nyama ya Punda na Vibudu linafanywa na vishoka ndio maana tumeanzisha utaratibu wa kuwasajiri wauzaji wa Nyama ili kudhibiti hali hiyo” Amesema

Naye Mwanasheria wa Bodi hiyo Pressgod Lukio amesema kuanzia sasa bodi hiyo itaanza kuchukua hatua kwa kuwafikisha mahakamani baadhi ya wauzaji wa Nyama wasiozingatia taratibu za Nyama  katika viwanda vya Nyama na machinjio.
 
“Sheria imeelekeza atakayefanya biashara ya Nyama haramu kwa kumlisha mlaji nyama Asiokula bila ridhaa yake atakamatwa na kufikishwa mahakamani na kifungo chake kinaanzia miaka mitatu na faini isiyopungua milioni 5 ama vyote kwa oamoja na kuendele”Amesema
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )