Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 16, 2018

Hukumu ya Wema Sepetu yasogezwa mbele

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu hadi Julai 20, 2018 siku ya Ijumaa kwa ajili ya kutoa  hukumu juu ya kesi hiyo.

Hukumu hiyo ilipaswa kusomwa leo lakini imesogezwa mbele hadi Julai 20 kutokana na hakimu anayesikiliza shauri hilo kutokamilisha kuandika hukumu.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Julai 16, 2018 na  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

“Naomba mniwie radhi kuna vitu vichache bado sijaviweka katika hukumu yangu, hivyo naomba kuiahirisha hadi Julai 20, ili niweze kuvikamilisha,” amesema hakimu Simba.

Hukumu hiyo inatarajia kutolewa Julai 20 baada ya mawakili wa upande wa utetezi, Albert Msando na wa mashtaka, Costantine Kakula kuwasilisha hoja za majumuisho katika kesi hiyo.

Tayari mashahidi watano wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi, mahakama hiyo kuwaona  washtakiwa kuwa na kesi ya kujibu na walianza kujitetea.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  wafanyakazi wake Angelina Msigwa (23) na Matrida Abas (19) ambao wote kwa pamoja  wanakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bhangi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )