Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, July 28, 2018

Jeshi la Polisi Jijini Mwanza Lakamata Sila 4 na Jambazi Moja

Mnamo tarehe 26/07/2018 majira ya saa 21:00hrs usiku katika mtaa wa bugarika wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza. Mussa faustine, miaka 19, mkazi wa mtaa wa bugarika, alikamatwa na wananchi na kupigwa sana, hii ni baada ya kuwatishia kuwapiga kwa bastola iliyotengenezwa kienyeji wananchi wale, ndipo wakati wakiendelea kumpiga taarifa zilifikishwa polisi ambapo askari waliokuwa doria walikwenda haraka  kutoa msaada na kumuokoa kijana huyo huku akiwa na silaha hiyo na risasi saba za silaha aina ya short gun. 

Pamoja ya kwamba alikuwa katika hali ya kipigo ilibidi askari waondoke nae na kwenda kumhoji vizuri wapi alilopata hiyo silaha, anafanya shughuli gani na anashirikiana na nani.

Kijana huyo alitoa ushirikiano vizuri kwa askari japo alikuwa katika hali ya kujeruhiwa sana, alitoa ushirikiano na kueleza kikundi chake ambacho wanashirikiana katika kufanya na kupanga matukio ambayo walikuwa wamepanga kufunya katika siku za hivi karibuni kisha alimtaja kiongozi wake aitwaye hamza @ mjomba. 

Katika maelezo yake tuliweza gundua kwamba hamza huyu ni  mmojawapo mwa wale majambazi waliokuwa wametoroka katika tukio la tarehe 08.7.2017 , ambapo katika tukio lile waliweza kuuawa majambazi wapatao saba huko maeneo ya fumagila.

Pia kijana huyu alitueleza kuwa hamza amerudi tena mwanza na sasa ivi wameanza kujipanga tena ili waweze kufanya matukio mengine zaidi, lakini pia aliwataja watu wengine wanao wawezesha kifedha ili waweze kufanikisha mambo yao wanayoyapanga, majina yao tunayo tutayashughulikia kwa kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ili tuweze kuwahoji na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Sambamba na hilo kijana huyo tuliweza kumhoji kama anazo silaha nyingine na yeye alitoa ushirikiano vizuri na alieleza zilipokuwepo tulikwenda nyumbani kwake na kuweza kupekua na kukuta silaha nyingine mbili zilizo tengenezwa kienyeji. 

Vilevile alitupeleka kwenye nyumba nyingine iliyopo eneo la kisesa ambapo ndipo alipokuwa anakaa hamza napo ilipatikana silaha nyingine moja, jumla zilipatikana silaha nne na risasi saba za silaha aina ya short gun. 

Lakini kwa taarifa alizotupa alisema wanazo silaha nyingine, ndio maana sasa tunafanya juhudi kubwa za kumtafuta kiongozi wao hamza pamoja na kundi lake  ili tuweze kusambaratisha kikundi hicho.

Pia tulikuta makaratasi yaliyochorwa namna ya kutengeneza silaha, tumepata habari kuwa kundi hili ndilo linalochukua watoto na kuwapeleka huko wanapokujua wao wenyewe na kuwafundisha namna ya kutumia silaha ili kuja kufanya uhalifu hapa mwanza na maeneo mengine katika nchi yetu. 

Aidha wakati tulipoona kijana huyo hali yake inazidi kuwa mbaya tulimpeleka hospitali kupatiwa matibabu lakini baadae alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza hususani vijana akiwataka kuacha kujihusisha na uhalifu tena uhalifu wa kutumia silaha kwani matokeo yake yanaweza yaweza kuwa kifo, kilema cha maisha au kufungwa, hivyo vijana wafanye kazi zilizo halali za kujiongezea kipato na sio vinginevyo. Vilevile anawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kama walivyofanya wananchi wa mtaa wa bugarika.

 IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )