Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, July 24, 2018

JUKATA Wataja Vikwazo 9 Uchaguzi 2020

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali kufanya marekebisho ya sheria na Katiba ya nchi yanayoendana na mahitaji ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Julai 23, 2018 jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alitaja maeneo tisa yanayohitaji mabadiliko ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wenye haki.

“Kutokana na kwamba serikali ya awamu hii imetamka kuwa mchakato wa katiba mpya sio kipaumbele chake, na kimesalia kipindi kifupi kufika mwaka wa uchaguzi tukiwa kama jukwaa la katiba tunashauri mabadiliko yafanyike haraka”. alisema Mwakagenda.

Mwakagenda alitaja maeneo yanayohitaji mabadiliko ya katiba zaidi kuwa ni, uhuru kamili wa tume ya taifa ya uchaguzi na tume ya uchaguzi ya Zanzibar, kuungana kwa vyama vya siasa, uwakilishi wa uwiano wa 50/50, mgombea binafsi aruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu, na matokeo ya Rais yahojiwe mahakamani,Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi zote na kurejesha ushindi wa rais kwa kura nyingi.
"Kama tunahitaji uchaguzi wa amani, mabadiliko hayo ni muhimu sana ili kuingia kwenye uchaguzi kwa amani, "alisema Mwakagenda.

Historia ya kuandikwa kwa Katiba Mpya ilianza Desemba mwaka 2011 wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akilihutubia taifa na baadaye aliwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba, ambayo ilianza kazi yake Mei 3, mwaka 2012.

Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kuandaa Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotolewa Juni 4, 2013 kabla ya kutoa Rasimu ya pili ya katiba hiyo iliyoendelea kujadiliwa bungeni, huku wabunge wa upinzani wakisusia vikao hivyo ndipo lilipoibuka jina UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi), Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili, lakini haikufanikiwa kukamilisha mpaka awamu ya Rais Kikwete ilipomalizika.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )