Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Kangi Lugola: Wizara Yangu Haihusiki na Mambo Ya Watu Kupotea

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vyombo vya usalama havishughuliki na kutoweka kwa watu bali wanahusika na watu waliotendewa uhalifu.

Lugola ameyasema hayo leo Ijumaa Julai 6, katika mkutano wake na waandishi wa habari na wakuu wa vyombo vya usalama wakati alipoulizwa kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari, Azory Gwanda.

“Kuhusiana na watu kutoweka, sisi Wizara ya Mambo ya Ndani hatuingilii uhuru wa ndani wa mtu, huyo ambaye mnasema ametoweka nyumbani kwake sisi hatuhusiki, kwa sababu kuna mwingine anatoweka kutokana na sababu za kimaisha,” amesema.

Waziri Lugola alisema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.

“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema.

Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati  akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

"Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka,"
alisema Lugola

Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Lugola amemtoa kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza kwa kuchelewa kikaoni huku akiahirisha kikao chake na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na idara zilizopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na kutokuja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano waliopanga kuufanya baada ya mazungumzo na waandishi wa habari na kuwaagiza wakuu wa majeshi wakachukue ilani ndipo warudi kuendelea na kikao.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...