Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 2, 2018

Kigwangalla Akabiliana na Majangili Msituni

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanikiwa kutaifisha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu katika pori la msitu wa Patamela baada ya kuhofia kukamatwa.

Hayo yamebainishwa na Waziri Kigwangalla ambaye yupo katika ziara ya pori kwa pori mkoani Songwe ambapo amebainisha kuwa baada ya wahalifu hao ambao walikuwa wakifanya ujangili katika machimbo ya madini walichoma moto na kutelekeza vifaa vyao kisha kutoroka.

Akisimulia tukio Waziri amesema " Kwenye ziara yetu wilayani Songwe, Mkoa wa Songwe, kwenye msitu wa Patamela, ambao ni msitu wa asili wa hifadhi wa kitaifa unaochukua sehemu kubwa ya wilaya za Songwe na Chunya, tulikuta kuna ujangili wa uchimbaji madini ulioshamiri, wahalifu walichoma moto ili kutuchelewesha tusifike eneo la tukio waweze kuondoka".
 
Ameongeza, "Bahati nzuri, tulipambana kwa ushirikiano wetu wote tuliokuwepo na tulifanikiwa kuudhibiti moto na kuendelea na safari mpaka eneo lililovamiwa na wachimbaji haramu wa madini. Tuliwawahi wakakimbia wakatelekeza vifaa na mashine (wheel loader) ambayo tumeitaifisha, sambamba na makinikia yote".

Hata hivyo Kigwangalla amesema kazi  bado inaendelea na ziara ya pori kwa pori inaendelea ambapo leo atakuwa Chunya mkoani Mbeya.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )