Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 2, 2018

Nassari Akana Kumshambulia Mwigulu Nchemba

Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amekataa tuhuma za kumshambulia kwa maneno, katika mitandao ya kijamii aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Nassari ametoa kauli hiyo leo na kudai kuwa hatumii akaunti hiyo twitter na amejaribu kufuatilia anayetumia jina lake kwenye mtandao huo kufanya vitu ambavyo hata yeye hapendezwi navyo lakini hajafanikiwa.

“Situmii hiyo akaunti twitter na siyo mara ya kwanza mwenye hiyo akaunti kuandika vitu vya ajabu ambavyo havinihusu na nimejaribu kumtafuta mara kadhaa lakini sijafanikiwa, bora angekuwa anaandika hata mambo ya kilimo ningemuona ana akili”, amesema Nassari.

Ikiwa imepita siku moja tangu kutangazwa kwa mabadiliko ya baraza la Mawaziri huku Mwigulu akiachwa, kupitia ukurasa wa ‘twitter’ wa mtu anayejiita Joshua Nassari ameandika ujumbe uliosomeka kuwa, “Kutumbuliwa kwa Mwigulu hakumsafishi kwa wananchi”.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...