Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, July 3, 2018

Rais Magufuli: Ni Marufuku Kuwahudumia Wafungwa Bura, Wafanye Kazi

Rais Dkt. John Magufuli ametoa agizo kwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, aliyeapishwaa jana Kangi Lugola kuwa anapaswa kuanzisha mpango madhubuti wa kusimamia na kuwatumia wafungwa katika mpango kazi wa kilimo, na sio kuwalea magerezani.

Akizungumza jana katika hafla ya kuwaapisha viongozi walioteuliwa,alimwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuhakikisha wafungwa wote nchini wanafanyakazi katika mashamba ya kilimo ili kuzalisha chakula kwa faida ya nchi.

“Haiwezekani Tanzania ikawa ni nchi ya kupoteza fedha nyingi kuwahudumia wafungwa na kupata hasara wakati Nchi za wenzetu wanatumia wafunga katika shughuli za uzalishaji”, alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli aliongeza kuwa suala la muda upi wa wafungwa kufanya kazi, atajua mwenyewe iwe usiku au mchana, anachotaka yeye ni kazi tu.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )