Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, July 24, 2018

Salamu za Pongezi za Mhe. Rais Magufuli kwa Rais Filipe Nyusi na Wananchi wa Msumbiji.

Rais John Magufuli ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi  wanachama wa Frelimo na wananchi  wa nchi hiyo ambao kesho Jumatano Julai 25, 3018 wanaadhimisha miaka 50 ya mkutano wa pili wa chama hicho.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Julai 24, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema katika sherehe hizo zitakazofanyika Matchedje katika jimbo la Niassa, Rais Magufuli atawakilishwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na makamu mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.

Katika salamu zake, Magufuli amewatakia heri wananchi wote wa Msumbiji na kuwapongeza kwa mafanikio waliyoyapata ikiwemo kudumisha uhuru wao.

Amesema Tanzania inajivunia uhusiano, historia na ujirani mwema na nchi hiyo.

“Kwa niaba ya Serikali, CCM na watanzania wote naungana nawe (Nyusi) na wananchi wote wa Msumbiji katika kusherehekea siku hii muhimu,” amesema Rais Magufuli.

“Siku hii inatukumbusha jukumu muhimu tulilonalo la kuulinda na kuutetea uhuru ambao waasisi wa mataifa yetu Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Samora Machel wa Msumbiji waliupigania.”

Rais Magufuli amemhakikishia Nyusi kuwa Tanzania  itaendelea kudumisha na kukuza uhusiano wake na Msumbiji katika ngazi ya Serikali na vyama vya CCM na Frelimo, kuimarisha ushirikiano hasa katika masuala ya uchumi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )