Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, July 4, 2018

Sharti Walilopewa Mtibwa Sugar na CAF Ili Waweze Tena Kushiriki Michuano ya Kimataifa

Shirikisho la soka nchini (TFF), kupitia kwa Katibu mkuu wake Kidao Wilfred leo wameweka wazi kuwa, wanalishughulikia suala la faini waliyopigwa Mtibwa Sugar na CAF na watahakikisha timu hiyo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa.

Akizungumza na wanahabari leo, Kidao amesema wamepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF inayoelezea klabu ya Mtibwa kumaliza adhabu yake ya kufungiwa lakini ikitakiwa kuthibitisha kwa maandishi malipo ya faini ya dola 1500 na fidia kwa klabu ya Santos ya Africa Kusini.

''Suala la Mtibwa Sugar na faini waliyopigwa na CAF mwaka 2003 ya dola za Kimarekani 1500, tunalifanyia kazi na tutajitahidi kuhakikisha faini hiyo inalipwa kabla ya Julai 20 ili timu hiyo iweze kushiriki kwani tayari CAF wamethibitisha kuwa wamemaliza adhabu hiyo kilichobaki ni uthibitisho wa maandishi tu kuhusu malipo hayo'', amesema Kidao.

Mwaka 2003, Mtibwa Sugar ilipigwa faini na CAF pamoja na kufungiwa kutoshiriki michuano yoyote inayosimamiwa na shirikisho hilo kwa misimu miwili, kutokana na kushindwa kwenda kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Santos FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo wa kwanza hapa nyumbani Mtibwa Sugar ilifungwa mabao 3-0.

Hata hivyo kwa mujibu wa uongozi wa Mtibwa Sugar wao wanadai wameshalipa faini hiyo, kipindi ambacho Shirikisho la soka lilikuwa linaitwa FAT. Kidao amesema wao kama TFF hawajaziona rekodi hivyo itawalazimu kuwasiliana na CAF ili kujua kama faini hiyo ililipwa.

Mara ya kwanza kwa Mtibwa Sugar kushiriki michuano ya Kimataifa ilikuwa mwaka 2001, kisha ikashiriki tena 2002 na mara ya mwisho ilikuwa ni 2003, ambapo ikafungiwa hiyo miaka miwili na faini.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )