Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 13, 2018

Shule ya Sekondari Magufuli yaongoza kimkoa matokeo kidato cha sita

Shule ya Sekondari Magufuli iliyopo wilayani Chato, Geita imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya shule 10 zilizopo mkoani hapa.

Shule hiyo pia imeshika nafasi ya 18 kitaifa ambapo watahiniwa wote 82 wamefaulu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Julai 13, wanafunzi 40 kati yao wamepata daraja la kwanza 40 wengine daraja la pili na wawili daraja la tatu.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joel Hari amesema shule hiyo imeonyesha juhudi kwani mwaka jana ilishika nafasi ya pili kimkoa na kitaifa ilishika nafasi ya 28.

Mbali na shule ya Magufuli pia shule ya wasichana ya Jikomboe ya wilayani humo imeshika nafasi ya nne kimkoa huku shule ya Chato ikishika nafasi ya saba kimkoa.

Hari amewapongeza walimu na idara ya elimu sekondari katika wilaya hiyo kwa jitihada kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanafunzi wanafaulu.

Wilaya ya Chato ina shule 27 za sekondari ambapo kati ya hizo shule tatu ni za kidato cha tano na sita.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )