Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, July 21, 2018

Taarifa kwa Umma: Barabara ya Nelson Mandela Imefungwa kwa Siku 3 tangu Jana

 Kuanzia jana  Ijumaa Julai 20, 2018 hadi Jumatatu Julai 23, 2018 watumiaji wa barabara ya Nelson Mandela jijini Dar es Salaam watakumbana na usumbufu kutokana na matengenezo yatakayoanza kufanyika katika barabara hiyo eneo la Ubungo.

Kufuatia matengenezo hayo, kuanzia  eneo la mataa ya Ubungo hadi Riverside (kama unatokea Mwenge kuelekea Buguruni), itafungwa kwa siku hizo, badala yake magari yatalazimika kupita upande wa pili wa barabara hiyo hiyo (inayotoka Buguruni kuelekea Ubungo).

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa Julai 20, 2018 na kampuni ya CCECC inayojenga barabara za juu katika makutano ya Ubungo.

“CCECC inapenda kuwajulisha watumiaji wa barabara katika makutano ya Ubungo kuelekea Nelson Mandela (Riverside) kuwa siku ya Ijumaa Julai 20 kuanzia saa tano usiku hadi Jumatatu (Julai 23) ujenzi utakuwa unaendelea na watumiaji wa barabara hii watakuwa wanapita kama inavyoonekana kwenye mchoro huu,” imesema taarifa hiyo.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )