Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 19, 2018

VIDEO: Maamuzi ya TCRA Kwa Hamisa Mobeto na Irene Uwoya Baada ya Kuweka Picha za Nusu Uchi Mtandaoni

Msanii Irene Uwoya  na Mwanamitindo Hamissa Mobetto wamewajibishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA  kwa kosa la kuweka picha za Nusu uchi mitandaoni kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018.

Katika maamuzi yake na kwa kuzingatia utetezi wa Hamissa Mobetto ambaye amesema picha hizo alizipiga mwaka jana nchini Kenya, TCRA  imempa Onyo la mwisho na kwamba akirudia, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, TCRA imemtaka Hamissa Mobetto kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram la kuwaomba msamaha watanzania na kuwataka kutosambaza picha zake za nusu uchi.

Kwa upande wa Irene uwoya, yeye pia kapewa Onyo la mwisho kwa kuzingatia utetezi wake alioutoa, pia ametakiwa kuomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

==>>Zaidi, tazama hapo chini
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )