Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 26, 2018

Wema Sepetu asema atajaribu kuwa na roho mbaya ili afanikiwe

Msanii wa filamu Wema Sepetu amedai kwa sasa anajaribu kujifunza kuwa na roho mbaya kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vyake vingi vimekwama kutokana na kuwa na roho ya huruma. 

Muigizaji huyo amedai watu wengi wenye roho mbaya wamefanikiwa zaidi kuliko wale wenye wema ambao hutumia maisha yao kusaidia marafiki zao.
 
Hata hivyo wema anasema kuwa kwa upande wake yeye inakuwa ngumu kuwa na roho mbaya kwa sababu mungu anakuwa tayari amekuumba hivyo hivyo huwezi kubadilika hata kidogo katika hilo.

Lakini amesema kuwa na yeye atajitahidi kuwa na roho mbaya ili aone kama inawezekana kufanikiwa kama wengine.

"Wanasemaga watu wenye roho mbaya wanafanikiwa sana, na mimi roho hiyo sina kwa sababu ninachoamini ni kwamba kama umejariwa roho nzuri basi hiyo ni roho yako tu huna haja ya kuwa na roho nyingine, sometimes roho yangu nzuri inaniponza sana.ila nitajitahidi kujifunza roho mbaya.

Akiongelea kuhusu kesi yake iliyoisha hivi karibuni wema ansema hana la kusema zaidi ya kumshukuru mungu kwa kuwa kipindi icho alikuwa katika wakati mgumu wa kufanya mambo mengi kwa kusua sua.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )