Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 20, 2018

Wema Sepetu Kafanikiwa Kulipa Faini na Kukwepa Kifungo

Msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu  amelipa faini ya Sh2milioni na kuepuka kifungo cha mwaka mmoja jela. 

Wema amelipa faini hiyo leo Ijumaa Julai 20, 2018 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kulipa faini ya Sh1milioni kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Wakati Wema akikutwa na hatia, washatakiwa wenzake ambao ni wafanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa na Matrida Abbas wameachiwa huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya dakika 45,  Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema upande wa mashtaka umeleta mashahidi watano, ambao walithibitisha mashtaka hayo.

Amesema baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake, washtakiwa wote walikutwa na kesi ya kujibu  na walijitetea wakiongozwa na wakili wao,  Albert Msando.

"Nawaachia huru mshtakiwa wa pili na wa tatu kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao lakini kwa upande wa Wema hakuna shaka lolote kwamba alipatikana na dawa za kulevya,” amesema hakimu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )