Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, August 5, 2018

Ajali yaua wanafunzi 9.....Kenyatta Aomboleza

Wanafunzi tisa wa Shule ya msingi ya St. Gabriel huko Mwingi, Kaunti ya  Kitui nchini Kenya, wamefariki huku  wengine 32 wakiwa wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi ya shule na lori usiku wa Jumamosi kuamkia leo.

Wanafunzi nane wametajwa kufariki katika eneo la ajali hiyo huku mmoja ambaye anaongeza idadi ya kufika tisa amefariki akiwa hospitali ya taifa wakati anapatiwa matibabu.

Wanafunzi hao walikuwa wakitokea Mombasa kwenda katika safari ya kimasomo ambapo basi lao liligongana uso kwa uso na Lori katika daraja la Kanginga, Kilomita moja kutoka mji wa Mwingi kwenye barabara ya Thika-Garissa usiku wa manane.

Aidha kati ya majeruhi 32 ya wanafunzi ya waliofikishwa katika Hospitali ya Mwingi, wanafunzi Sita wanadaiwa kuwa katika hali mbaya (mmoja amefariki na kubaki watano)  ambapo wameshahamishwa katika hospitali ya Taifa ya Kenya, (Kenyatta National Hospital).

Wanafunzi nane waliofariki ni kati ya abiria 50 waliokuwa kwenye basi hilo pamoja na walimu.

Katika ujumbe wake kwa wazazi na walezi wa wanafunzi, Rais Kenyatta amesema ni bahati mbaya kwamba maisha ya wanafunzi wasio na hatia yamekatisshwa na kwamba  "Tumewapoteza wale ambao tulitegemea kujenga nao taifa siku za usoni".

Aidha Dereva wa lori hilo tayari amekwishakamatwa na Jumatatu atafikishwa mahakamani.


Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )