Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 8, 2018

Breaking News: Mzee Majuto Afariki Dunia

Mchekeshaji mkongwe nchini mzee Majuto amefariki dunia leo Agosti 8  saa mbili usiku huu baada ya kulazwa siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mtoto wake aitwaye Abuu amethibitisha habari hizi. Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram.

“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” aliandika Joti.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )