Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 28, 2018

Mtawa afariki dunia baada ya kujirusha kutoka Ghorofani

Mkurugenzi wa fedha na mipango wa hospitali ya Rufaa Bugando, Mtawa Suzan Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa kamili atazungumza na waandishi wa habari baadaye.

Kwa mujibu wa ofisa uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele amesema kuwa Mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumzia suala hilo na kutaka litafutwe shirika la Watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba mkoani Kagera.

“Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala hilo,” amesema Lucy
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )