Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 21, 2018

Mwinyi Mgeni rasmi mashindano ya mashairi ya Meya wa jiji la Dar.

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili ,Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mashairi ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita yatakaofanyika Septemba moja na  mbili mwaka huu katika ukumbi wa Karimu Jee.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, kwa niaba ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Mratibu wa mashindano hayo ,Shehe Mwita Kambi amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kukuza lugha ya Kiswahili hapa nchini.

Amefafanua kuwa washiriki wa mashindano hayo ni wakazi wa jijini hapa ambapo kila mmoja atapaswa kutunga shairi lisilozidi beti nane na kupungua beti kumi.

Mashindano hayo  ya mashairi ambayo hufanyika kila mwaka ,hukusudia  hukutanisha magwiji,wakongwe wa lugha ya Kiswahili na hivyo washindi kupatiwa zawadi ya fedha Tathilimu kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi bora.

“Lengo kubwa la mashindano haya ni kukuza lugha ya Kiswahili, ambayo ndio Lugha Mama, mtakubaliana na mimi kuwa viongozi wetu wa serikali ,akiwemo rais Dk. John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza lugha hii kwani wote ni mashahidi kwamba hata katika ziara zake za nje ya nchi amekuwa akihutubia kwa kutumia lugha ya Kiswahili” amesema Shehe Mwita.

Kutokana na umuhimu wa tukio hilo” Niwakaribishe wananchi wa jijini hapa kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo,mshindi wa kwanza atapatiwa fedha kiasi cha shilingi milioni moja, wapili shilingi laki tano, watatu shilingi laki tatu,na mshindi wan ne hadi wa kumi atapatiwa shilingi laki moja.

 Aidha mratibu huyo amesema kuwa ,ujumbe wa mwaka huu katika utungaji wa mashairi ni “LUGHA YETU,FAHARI YETU, huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza kampuni ya mabati ya ALAF kwa kuzamini mashindano hayo.

Kwaupande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Theresia Mmasy amesema kuwa lengo la kuzaminishi mashindano hayo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wa serikali katika kuhakikisha kwamba wanatangaza lugha ya Kiswahili hapa nchini na nje ya nchi.

Amefafanua kuwa kila mwaka wamekuwa wakiendesha mashindano hayo na kwamba mwaka huu wameona kuna tija ya kumuunga mkono Meya wa jiji la Da es Salaam kutokana na kuonyesha nia ya kukuza lugha hiyo.

Mwishoo.

Imetolewa leo Agosti 21 na Christina Mwagala, Afisa Habari Ofisi ya Meya wa jiji.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )