Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 8, 2018

Shibuda Amtaka Bashiru Ally Kuwadhibiti Wanaotafuta ‘kiki’

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,  John Shibuda, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally kuwadhibiti watumishi wa Serikali wanaoibua mambo na kuyatenda kwa kutafuta ‘kick’ za kisiasa kinyume na amri ya Rais John Magufuli.

Amesema tabia za namna hiyo zikiachwa zikazoeleka katika jamii na watu wakatambua kuwa yeye (Rais) ndiyo anatoa amri hizo kumbe siyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti 8, katika mkutano wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini, Shibuda amesema baadhi ya maagizo mengi yanayotolewa na viongozi si amri za Rais Magufuli.

“Namuomba Dk. Bashiru awadhibiti watumishi wa serikali wanaotafuta kiki za kisiasa kwa wanaoibua mambo ambayo hayana amri za Rais Magufuli na kujijengea umimi na usisi, mkiondoa hilo mtakuwa mnajenga taswira njema.

“Na msiache tabia zenye kujenga kasoro na kuibua hitilafu dhidi ya rais zikazoeleka ndani ya jamii na watu wakatambua kuwa yeye ndiyo anatoa amri hizo ila kwa ufahamu wangu naamini kuwa baadhi ya mambo yanayosemwa hayatoki kwake,” amesema Shibuda.

Amewataka watumishi hao kuacha kumbebesha mambo ambayo si ya kwake wakidhani kufanya hivo wataifurahisha jamii na kumfurahisha Rais Magufuli mwenyewe.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )