Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, August 25, 2018

Ugonjwa wa Dimpoz wamaliza tofauti yake na Diamond

Msanii Diamond Platnumz amezitupilia mbali tofauti zake zilizokuwepo kati yake yeye na msanii mwenzake Ommy Dimpoz katika wakati huu mgumu kwa Ommy Dimpoz na kumuombea apone mapema ili aweze kurudi katika hali yake ya mwanzo.

Diamond ameweka picha ya msanii mwenzake huyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akimwombea apone haraka na kurejea katika muziki.

“Inshaallah! Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi uweze kupona haraka na kurudi kuendelea na sanaa ili pamoja tuzidi kupeleka muziki wetu mbali zaidi,” ameandika Diamond.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyu kuweka ujumbe katika mtandao wake kuhusu  Ommy Dimpoz tangu walipojibizana katika vyombo vya habari Agosti, 2017 huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake mambo mbalimbali.

Dimpoz akiwa msanii chini ya lebo ya Rock Star 4000 pamoja na Alikiba, wamekuwa na uhasama wa kimuziki na Diamond Platnumz kwa muda mrefu.

Mashabiki wa Diamond wamempongeza kwa kuweka pembeni tofauti zao za kibiashara na kumpa pole mwenzake kupitia mtandao huo wa kijamii.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )