Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, September 2, 2018

Esma akana kwamba yeye na mama yake walikuwa wanaandaa Mpango wa Kumchafua Hamissa Mobetto

Dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka mtandaoni kukanusha madai ya kwamba yeye na mama yake walikuwa wanafanya audition kwaajili ya kumpata mtu mwenye sauti kama ya Hamisa Mobetto.

Kwa mujibu wa shabiki huyo wa Hamisa amedai wawili hao walifanya mpango huo kwaajili ya kuandaa sauti ambayo itatumika kumchafua mrembo huyo ambaye ni mzazi mwenza na Diamond Platnumz.

Esma ameona azijibu tuhuma hizo huku akidai kwamba yeye pamoja na mama yake hawawezi fanya kitu kama hicho kwa Mobetto.

“Dada bora ukae kimya halafu unapata zambi kumshilikisha Mwenyezi Mungu ktk swala km hili kuongopa vitu mbona sie wenyewe tupo Kimya au ndio mnatapatapa embu mjitulize jamani hata MUNGU HAPENDI kwani ye ndio Muamuzi plz naomba msinitungie uongo wa kijinga jinga mlichokifanya wenyewe mnakijua na nafsi zinawasuta sipendi kuniingiza ktk uongo wa kijinga msijisafishe kutaka kuchafua watu. Huyo huyo mama mnaotaka awapende kutwa mnachamba na kumtungia uongo naombeni mkitaka kuweka uongo wenu bora mniweke mimi sio mamaangu. MLICHOFANYA MNAKIJUA
#temporarypostšŸ™Œ#mfaMajiHamuishiKutapatapa,” aliandika Esma kupitia Instagram.

Aliongeza, “Katika maisha ni vema kukaa kimya pindi ukikosea na hasa ukijua wazi kuwa nimekosea ila ukijaribu kufuta au kusawazisha kosa kupitia njia za wasiogusa maisha yako ujue kosa linazaa kosa…Ungetulia maana watu wameshiba vielelezo na ushahidi 100%,”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )