Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 8, 2018

Kiwanda cha Kagera Sugar Chatoa Kodi ya bilioni 44 kwa Miaka mitatu

Na Jacquiline Mrisho –Maelezo
Kiwanda cha Sukari cha Kagera kimeilipa Serikali kodi ya jumla ya shilingi 44,461,815,798 katika kipindi cha miaka mitatu tangu 2015 hadi 2018.

Takwimu hizo zimetolewa jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Balozi Dkt. Diodorus Kamala lililohoji manufaa ya kiwanda cha Sukari cha Kagera kwa wananchi wa Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mwijage amesema kuwa tangu kiwanda hicho kibinafsishwe,faida na michango mbalimbali imepatikana ikiwemo ya kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari kutoka tani 15, 362 zilizozalishwa mwaka 2004/05 hadi kufikia tani 75, 568 mwaka 2017/18 ambapo uzalishaji huo umesaidia kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza bidhaa hiyo toka nje ya nchi.

“Mpaka sasa kuna wakulima 500 wanaolima eneo la hekari 5, 019 za miwa ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 wakulima hao waliweza kuzalisha tani 60,000 za miwa zilizowapatia kipato cha shilingi bilioni kuwepo kwa kiwanda hiki ni faida kwetu hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wa sukari kuendelea kuzingatia sheria za kuendesha biashara hiyo,”alisema Mwijage.

Waziri Mwijage ameongeza kuwa hadi kufikia mwaka 2018, kiwanda kimetoa jumla ya ajira 6,000, kimejenga hospitali yenye vitanda 78, kimechangia vifaa vya ujenzi wa madarasa, kimechimba visima vya maji, kujenga vyoo, nyumba za walimu pamoja na madawati.

Vile vile kiwanda hicho kimechangia ujenzi wa maabara na kutoa vifaa vya kufundishia kwa shule 23 katika Wilaya ya Misenyi, kimepanda jumla ya miti 20,000 katika eneo la kiwanda hicho pia kimejenga mtandao wa barabara zenye urefu wa Kilomita 1,250.

Aidha, Waziri Mwijage amefafanua kuwa kiwanda hicho kina utaratibu wa kuwatumia wakulima wa nje katika kulima miwa inayotumia hivyo inawaletea manufaa wakulima nchini kwa kulima mazao bora yenye tija.

Kiwanda cha Sukari cha Kagera ni kati ya Viwanda vilivyobinafsishwa katika miaka 90 kikiwemo cha  Kilombero kilichopo mkoani Morogoro. Hivi karibuni Mhe. Rais John Pombe amekuwa akisisitiza kuwa viwanda vilivyobinafsishwa na  hadi sasa havifanyi kazi virudishwe Serikalini.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )