Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 1, 2018

Muna Love kutoa kitabu cha Maisha ya Patrick

Msanii wa Filamu Bongo, Muna Love amesema kuwa ana mpango wa kutoa kitabu cha maisha ya mwanae Patrick aliyefariki.

Muna amesema hayo jana akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha William Malecela a.k.a Lemutuz kiitwacho My American Experience.

"Unajua ukishakuwa kwenye wokovu msiba pia ni furaha, hakuna mtu ambaye ataishi milele. Nahitaji kutoa kitabu changu cha mimi na Patrick," alisema Muna.

Mtoto Patrick alifariki July 03, 2018 akipatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya na alizikwa July 07, 2018 Dar es Salaam, Tanzania.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )