Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, September 27, 2018

Mwanafunzi Kortini Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi Mwenzie

adv1
Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Mbezi (19), Juma Idd  jana Jumatano Septemba 26, 2018 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 14.

Mwanafunzi aliyepewa ujauzito wenye miezi mitano sasa anasoma shule ya msingi Kunduchi na tayari ameshaanza kliniki katika zahanati ya Tegeta.

Akisoma shtaka hilo jana mbele ya hakimu Joyce Mushi, wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai tarehe tofauti kuanzia Aprili hadi Septemba mshtakiwa alimwingilia kimwili mwanafunzi huyo huku ukijua ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana kosa na wakili Makakala aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika, kumuomba hakimu apange tarehe nyingine.

Hakimu Mushi alimweleza mshtakiwa huyo kuwa dhamana yake iko wazi kwa kuwa shtaka hilo linalomkabili linadhaminika.

Hivyo Hakimu Mushi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa na kila mmoja atasaini bondi ya Sh1 milioni, masharti ambayo mshtakiwa huyo aliyatimiza na kuachiwa huru kwa dhamana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )