Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, September 18, 2018

Rosa Ree Akiri Kuacha Pombe Baada ya Kuona Haina Nafasi Katika Maisha Yake.

Msanii wa hiphop, Rosary Robert ‘Rosa Ree’ ameamua kuachana na ulevi wa pombe baada ya kugundua haina faida katika maisha yake.

Msanii huyo anayefanya vizuri kwa sasa, alisema Dar es Salaam juzi kuwa ameamua kuacha pombe maana haikuwa ikimnufaisha na chochote zaidi ya kufanya baadhi ya mambo yake yasiende vyema.

“Unajua pombe ukiipa nafasi kubwa ya kutawala maisha yako hautaweza kuiacha hata mara moja, ila wewe ukiitawala pombe unaweza kuiacha na ndio maana hata mimi niliweza,” alisema Rosa Ree.

Aidha, alishauri wasanii wenzake kuacha pombe kwani mara nyingi imekuwa ikipoteza muda na kushindwa kufanya mambo ya msingi.

Hatua ya msanii huyo kuacha pombe na kutangaza hadharani ni jambo la kupongezwa kwani wasanii wengi wameshindwa kuachana na kilevi hali inayosababisha wengine kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )