Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 12, 2018

Serikali Yawaagiza Wakurugenzi Nchi Nzima Kuwakamata na Kuwashitaki Watroto OmbaOmba

Serikali imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri na majiji kuwakamata watoto wanaombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro shuleni ikiwa ni pamoja na wazazi wao.

Agizo hilo limetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda wakati akijibu swali la Mbunge wa Kiembe Samaki Ibrahim Raza, ambaye alihoji ni lini serikali itachukua hatua kuwaondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam, ambaye amekiri kuwa ombaomba bado ni tatizo katika jiji hilo.

Naibu Waziri Kakunda ameema ombaomba wengi wanakwenda Dar es Salaam kwa sababu vipo vivutio vingi ikiwemo watu wenye imani mbalimbali ambao huwapatia fedha na vitu vingine kama sehemu ya ibada.

"Ombaomba wamekuwa wakirudishwa makwao lakini wanarejea tena, hii inathibitisha kuwa wapo watu wazima wanaowatumia watoto kuomba, nawaagiza wakurugenzi kuwakamata watoto wote wanao ombaomba mitaani ili washtakiwe kwa mujibu wa sheria inayokataza utoro mashuleni,” amesema Kakunda.

Aidha, Kakunda ameliambi bunge kuwa kuzagaa kwa ombaomba kumekuwa chanzo kimoja wapo cha uchafuzi wa mazingira katika Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewahi kuendesha zoezi la kuwakamata na kuwarejesha makwao ombaomba wanaozagaa Jijini huku akitoa agizo kwa jamii kuachana na huruma ya kutoa misaada ya fedha kwa watoto ambao wanarandaranda mitaani kwa kuomba fedha katika maeneo mbalimbali nchini kwakuwa wamekuwa wakitumiwa na wazazi wao.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )