Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, September 22, 2018

Sister Fey Atiwa Mbaroni Kwa Matumizi Mabaya ya Mtandao

adv1
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Faidha Omary maarufu kama Sister Fey amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kukiuka maadili kwa kuchapisha maudhui yanayodhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza  ambaye amesema  kuwa aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kumfuatilia msanii huyo juu ya matumizi yake ya mitandao na mwishowe waliweza kumkamata Septemba 19, 2018 usiku na kumuweka kituo cha polisi mabatini ambapo kwa sasa anasubiriwa kupandishwa Mahakamani.

"Mchakato wa kumchukulia hatua Sister Fey umeanza muda mrefu na kimsingi mimi kama Naibu wa Waziri ambaye nipo katika wizara inayosimamia masuala ya sanaa likiwepo na suala zima la maadili kwasababu vitu ambavyo alikuwa anavifanya Fey kila mtanzania alikuwa anaviona na vitu ambavyo vipo kinyume na maadili ya kitanzania", amesema Shonza.

Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema alitegemea kumuona Sister Fey kubadilika mwenendo wa tabia yake, pindi alipoitwa kwa mara ya kwanza na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lakini ndio kwanza alizidisha kufanya vitendo viovu.

"Naomba tu, niwaambie wasanii kiujumla wafuate taratibu na misingi iliyowekwa kwani endapo watakiuka sisi tutaendelea kuwakamata na kuwaweka ndani ili kusudi sheria iweze kuchukua mkondo wake", amesisitiza Shonza.

Sister Fey ni miongoni mwa wanamuziki walioweza kujipatia umaarufu mkubwa mitandaoni kwa vituko vyake visivyokuwa na maadili licha ya jamii kumkanya lakini yeye hakuweza kuacha na kuendelea kufanya hivyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )