Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, September 3, 2018

Swala la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye miradi ya ujenzi Lamkera Rais Magufuli...Atoa Wiki Moja kwa Waziri wa Fedha

Rais John Magufuli ametoa muda wa wiki moja kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na mwenzake wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe kumaliza tatizo la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwenye  miradi ya ujenzi akisema inachelewesha na kukwamisha miradi.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jijini Mwanza leo Septemba 3, 2018 wakati akihutubia wananchi baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya kujenga meli mpya, Chelezo na ukarabati wa meli mbili za Mv Butiama na Mv Victoria.

"Suala la msamaha wa VAT ni kikwazo kwa miradi ya maendeleo. Unakuta miradi iko tayari kutekelezwa lakini linakuja suala la VAT linakwamisha," amesema nakuongeza: "Waziri (wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi), kaeni na Waziri wa Fedha mlimalize hili na limalizike ndani ya wiki moja."

Rais Magufuli yuko kwenye ziara ya kikazi katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza, Mara na Simiyu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )