Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 26, 2018

Watu Zaidi Ya 1,500 Watakiwa Kuhakiki Silaha Zao Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amewataka wamiliki zaidi ya 1,500 kuhakiki uhalali wa umiliki wa Silaha zao na kutakiwa kujisalimisha polisi kabla ya masoko dhidi yao kuanza

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa  msako mkali kwa watako kaidi agizo hilo utafanyika katika wilaya zote na vitongozi vyake

“Kuna zaidi ya watu 1500 wanaomiliki silaha zikiwemo bastola, shotgun na rifle. Waje kwenye vituo vya polisi mkoani au wilayani kuhakiki uhalali wa umiliki wa silaha zao na kusema kuwa Majina yao tunayo. Tunataka kujiridhisha uhalali wa umiliki wao pamoja na kutakiwa kulipa tozo halali ya serikali.

Aidha Kamanda huyo ametangaza kuuawa kwa majambazi wanne waliomvamia mfanyabiashara mkazi wa kijiji cha Maziwa, Tarafa ya Farkwa na kumuibia sh. milioni moja ya mauzo ya duka.

Katika tukio hilo wananchi walianza msako dhidi ya majambazi hao na walipofika kwenye kijiji cha Kitalalo, wilayani Manyoni mkoani Singida, walibaini majambazi watatu kati ya wanne wamejificha porini majira ya saa sita usiku.

“Jambazi aliyekuwa na bunduki iliyotengenezwa kienyeji alijaribu kuwafyatulia risasi lakini iligoma ndipo wananchi walipoanza kuwashambulia majambazi hayo hadi kuwaua,” alieleza.

SACP Muroto alibainisha kuwa baada ya polisi kufika eneo la tukio walikuta silaha moja aina ya shotgun na fedha taslimu sh. laki moja.

Katika tukio lingine, kamanda huyo wa polisi alieleza polisi imewakamata vijana wanne wakiwa wamechapisha noti bandia 3,181 za dola ya Kimarekani zikiwa kwenye sanduku na  pia walikamata kompyuta zilizowekwa program ya kudurufu noti bandia kwa kikundi cha vijana ambao wanaunda kikundi cha kisanii

“Kumezuka mtindo  wasanii pamoja na watu kutengeneza fedha bandia na kuzitumia kiholela mitaani na wengine kusingizia ni wasanii wanafanya sanaa.

Aliwataja waliokamatwa ni Amri Mtaki (21), Salim Hamis (19) Salmin Mohammed (22) na Asajile Mwakalinga (22) na kusema kuwa mtindo wa watu kutumia fedha kwa kuzidhalilisha haikubaliki na wahusika wote watakamatwa na kupandishwa mahakamani
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )