Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, September 7, 2018

Waziri Kigwangalla Aipokea Gold Ya Barnaba

Na Andrew Chale, Dar
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava Elias Barnaba maarufu kama kwa Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kukumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo jana Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajali Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu.

Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.

“Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee” alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.

Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu.

“Kwanza nikupe pole kwa ajali. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana” alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music.

“Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja” alisema Mxcater.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )