Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, September 27, 2018

Wizara ya Afya yawatahadharisha wananchi kuhusu akaunti feki inayotumia jina la Waziri wa Afya Kutapeli Watu

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekanusha vikali kuhusika na tangazo na umiliki wa ukurasa wa mtandao wa Facebook wenye chapisho la matapeli wa mtandaoni linalotangaza ajira za Shirika la Msalaba Mwekundu kwa watu 100 kila wilaya nchi nzima lilioandikwa TANZANIA RED CROSS JOB APPLICATION FORM.


Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika: “Huu ni UTAPELI, Sihusiki na Sijui lolote kuhusu Kazi za Red Cross, na nimewaomba TCRA kufuatilia na kuwachukulia hatua wahusika/matapeli hawa.”

Katika tangazo hilo, muombaji wa ajira anatakiwa kutuma pesa kiasi cha Tsh. 10,000/= wanazodai kuwa ni za uanachama na kuzituma kupitia M-pesa namba 0767291550 (yenye jina la Mr. Shabu Lifumike, Ofisa Muajiri Mkuu).
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )