Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, October 23, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 118 na 119 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 

Hawa taratibu akanisogelea hadi karibu na uso wangu, akanitazama kwa macho makavu yaliyo jaa ukakamavu, akavuta pumzi taratibu kisha akaishusha kwa nguvu na kukifanya kifua chake nione jinsi kinavyo shuka.
“Nakuruhusu kumuua baba yangu, ila nitaomba uwe mume wangu hadi kufa kwangu”
Sikutegemea Hawa anaweza kuzungumza maneno kama haya, jambo lililo nifanya nijawe na furaha na taratibu nikampiga busu la mdomo kumuhakikishia kwamba haya matatizo yakiisha nitakuwa mume wake wa maisha yake yote hadi pale kifo kitakapo tutenganisha.
       
ENDELEA   
“Nitakuwa, katika hili Mungu atuongoze”   
“Amen”
“Oparesheni yangu itaanza saa nane usiku nina amini muda huo watu watakuwa wamelala, na wewe ndio mtu wa pekee ambaye unaweza kuifanikisha hii oparesheni”
“Ndio ninaweza na nitakusaidia kwa kila jambo niwezalo, nitakupatia kinasa sauti, hakikisha kwamba tunawasiliana kwa kila hatua ambayo unakwenda kuifanya katika hii oparesheni”
“Sawa”
 
“Kikubwa hakikisha kwamba unamuanza Stive hao wengine watafwatia siku nyingine, sihitaji kuwe namauji ya mfululizo, wanaweza kunihisi mimi na watu wangu”
“Nimekuelewa mpenzi wangu”
“Kila kitu Dany ninafanya kwasababu ninakupenda, sikuhitaji kuuzika upendo wangu nilio nao juu yako, naamini huto niangusha katika hili?”
“Yaa sinto kuangusha”
Hawa akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu, akatoka chumbani hapa na kuniacha nikiendelea kuvipanga vitu vyangu kwa ajili ya kazi iliyopo mbele yangu. Hamu kubwa ya mauaji ikazidi kuutawala moyo wangu, sura za watu watatu ambao nimewapania kuwaua kwenye maisha yangu zinazidi kucheza kwenye fahamu yangu, kila sura inakuja kutokana na matukio yake waliyo nifanyia kwenye maisha yangu, japo Stive hajanifanyia mabaya ya moja kwa moja ila nimeweza kumgundua mapema sana.
 
Ilipo timu saa sita usiku nikaanza kuvaa mavazi yangu taratibu huku nikimsubiria Hawa kuweza kuja katika chumba changu, ili aweze kunipa taarifa ya kitu gani kinacho endelea ndani ya ngome hii. Nikamaliza kuvaa kila kitu huku upanga wangu mkali nikiuchomeka kwenye sehemu yake niliyo ivaa mgongoni mwangu. Bastola moja nikaichomeka kiunoni mwangu na bastola nyingine nikaichomeka kwenye buti ya mguu wa kushoto. Hadi inatimu saa nane kasoro usiku sikuweza kumuona Hawa, jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi, taratibu nikaanza kupandisha ngazi kuelekea kwenye mlamgo wa kutokea katika hichi chumba.
 
“Baba huo ni unyanyasaji, inawezekana vipi hadi munakagua chumba changu cha kulala ndani?”
Niliisikia sauti ya Hawa akifoka sana, na anaoenekana mtu anaye fokeana naye ni baba yake.
“Huu ni upelelezi endelevu nilazima tuwe na uhakika wa kujiridhisha, nilazima Dany atafute ninatambua atakuwa ndani ya hii ngome sehemu yoyote”
“Kwa hiyo baba sasa hivi imefikia hatua ya kuto kuniamini hadi unahitaji leo hii mimi kuchunguzwa?”
 
“Ni jukumu langu kulinda watu wangu, na siwezi kuona adui anaingia hadi kwenye himaya yangu na ninakaa kimya eti kisa ninampenda mwanangu wa kiume”
“Wewe kwenye kabati langu huko sihitaji mufungue, kuna nguo zangu za ndani”
Mapigo ya moyo yakaanza kunianda mbio kwa maana kabati katika chumba cha hawa lipo moja ambalo ndio hili lenye mlango wa siri wa kuingilia katika hichi chumba nilichopo mimi. Taratibu nikajikuta nikichomoa bastola yangu iliyopo kiunoni, nikaishika vizuri, na kujiapiza yoyote atakaye fungua mlango wa chumba hichi basi atatembelewa na malaika mtoa roho muda wowote.
“Kwa hiyo baba unahitaji kuona nguo zangu za ndani, basi acha nivue nguo uone uchi wangu, wewe si baba kwangu”
“Heii tokeni nje, tafadhali usivue mwangu”
Nilisikia sauti ya baba Hawa akizungumza kwa unyonge akionekana kutulia baada ya kujiwa juu na kutishiwa na mwanaye huyu.
 
“Samahani mwanangu kwa kukusumbua usiku huu”
“Baba mahusiano yako ya kimapenzi na Yudia yasiwe ni kigezo cha kunitelekeza mimi mwano, umesha nipokonya madaraka, kwangu hakuna kitu kingine kimya, niache niishi maisha yangu kwenye nyumba hii”
Nilimsikia Hawa akizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi, hapa ndipo nikaanza kupata ukweli kuhusina na kwa nini Yudia ameweza kumshusha Hawa kwenye madaraka yake kirahisi namna hiyo.
“Nani amekuambia mimi nina mahusiano na Yudia?”
“Baba unahisi ni siri ehee, ninakujua sana, laiti mama yangu angekuwepo wala haya yote yasinge nitokea mimi leo”
“Hawa rudi ulale mwanangu, usiku mwema”
Nikasikia vishindi vya viatu vikitoka chumbani kwa Hawa, kidogo nikajikuta nikishusha pumzi taratibu huku bastola yangu nikiirudisha kiunoni. Nikasimama kwenye ngazi hizi, hazikupita dakika hata tano mlango ukafunguliwa, Hawa alipo niona kwa haraka akanikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia kwa uchungu sana.
 
“Shiiiiii, ni kweli baba ana mahusiano na Yudia?”
“Ndio ni mwaka sasa na miezi yake”
“Pole sana”
Tukarudi chumbani kwa Hawa, akawasha taa yake na kunitazama jinsi nilivyo vaa. Taratibu akaanza kuipitisha mikono yake kwenye kifua changu kilicho funikwa na jaketi la kuzuia risasi.
“Dany kila kitu ninakiacha mikononi mwako, hakikisha kwamba unawaangusha maadui wako ambao kwangu kwa sasa pia ni maaduia”
Hawa alizungumza kwa kujikaza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Nimekuelewa”   
Tukaanza kunyonyana lipsi zetu huku kila mmoja akionekana kuwa na hisia kali moyoni mwake. Tukaachia Hawa akafungua droo ya meza yake, akatoa kinasa sauti kidogo, taratibu akakiingiza kwenye sikio langu, naye akachukua kinasa sauti kingine na kukivaa sikioni mwake.
“Hapo unanisikia?”   
“Yaa”
“Nitakaa kwenye computer hapa, nitahakikisha kwamba ninacheza na kamera zote za ulinzi za humu ndani ya ngome”
 
“Sawa umeweza kutambua ni wapi Stive alipo?”
“Sijatambua bado, ila ngoja”
Hawa akanyanyuka kwenye kiti, akazima taa, kisha akatoka chumbani kwake, baada ya dakika akarudi na kukaa kwenye kiti chake.
“Wapelelezi wangu wanasema yupo kwenye oparesheni ya kukutafuta hivi sasa”
“Si atakuwa na simu sehemu alipo?”
“Yaa”
“Unaweza kuhack sehemu alipo kutumia satelaiti”
“Hilo linawezekana ila inaweza kuwa hatari kwangu kwa maana chumba cha mawasiliano wakigundua kwamba ninadili na satelaiti wanaweza kunitilia msaka mimi pale mauaji yatakapo tokea”
“Sasa tunafanyaje, kwa maana nikisema nizunguke tu humu ndani nikiwa ninamtafuta yeye inaweza kuniletea shida na nitapoteza muda”
Sote tukajikuta tukikaa kimya tukitafakari ni kitu gani ambacho tunaweza kukifanya kwa muda huu.
“Ngoja”
Hawa akafungua droo ya meza yake, akatoa simu na kunikabidhi.
 
“Hii simu sijawahi kuitumia tangu niinunue, ina line na unaweza kuitafuta namba ya Stive kupitia simu hiyo, ukifanya mauji hakikisha kwamba unaiharibu simu huyo ili kuweza kufuta ushahidi”
“Nimekuelewa, nipatie namba yake”
Hawa kwa akatazama computure yaka kwa sekunde kadhaa kisha akanitajia namba ya Stive anayo itumia ndani ya hii ngome akiendesha msakao wa kunisaka mimi. Nikainakili namba ya simu ya Stive na kuiweka kwenye simu yangu.
“Nikutakie kazi njema mpenzi wangu”
Hawa akanipiga busu la mdomoni. Tukatoka hadi sebleni ambapo hapakuwa na mtu wa aina yoyote. Akawaomba walinzi wake walipo lindo nje ya nyumba yake waweze kupumzika kwa muda huu, pasipo wao wenyewe kuelewa ni kitu gani kinacho endelea.
 
“Ninazima taa ya nje, una sekunde ishirini kuondoka hapa sawa”
“Poa na hawa walinzi wako?”
“Nitawaambia nimebadili mawazo warudi kwenye nafasi zao za ulinzi”
“Ok”
Hawa akazima taa ya nje, kwa haraka nikakimbia kwenye eneo hili la uwazi na kujibanza kwenye jengo jingine ndani ya sekunde hizo ishirini alizo kuwa amenipatia. Nikatafuta sehem iliyo tulia katika hili jengo nikawasha simu hii, nikaanza kuitafuta namba ya Stive ni wapi alipo, haikuchukua muda mrefu nikafanikiwa kumuona, ila sehemu alipo ni mbali sana na mimi nilipo  kwa maana hii ngome ni kubwa sana.
 
“Dany unanisikia”   
“Yaa ninakupata”
“Umefanikiwa kumpata Stive?”
“Yaa nimefanikiwa kumpata, yupo geti la kusini”
“Ohoo God, so unafanyaje?”
“Nina dakika kumi kufika hadi huko alipo”
“Kumbuka kuna walinzi wengi hadi sehemu alipo”
“Yaa nalitambua hilo, nitahakikisha hadi inafika saa tisa kamili, kazi yangu hii nitakuwa nimesha imaliza”
“Kazi nje”
“Ok”
Tuliweza kuwasiliana vizuri na Hawa kwa kutumia vinasa sauti ambavyo vipo masikioni mwetu. Nikaanza kupita njia ambazo ninaamini kwamba hakuna mlinzi haata mmoja anaweza kuniona. Nikazidi kusonga mbele huku nikiwapiga chenga walinzi wanao endelea kunisaka kwa udi na uvumba, sikufahamu ni kitu gani ambacho wame ahidiwa kupewa pale watakapo nikamata kwa maana sikuwahi kuona msako mkali kama huu unao endelea katika hii ngome ya kundi la Al-Shabab ambalo linaogopewa karibia Afrika nzima na duniani.
 
“Dany”
Nilisikia sauti ya Hawa akiniita kwenye kipaza sauti, ikanibidi nisimame na kujibaza kwenye moja ya mti ili mradi niendelea kuzungumza na Hawa.
“Yaa”
“Mwenzio nina ogopa kwa kweli”
“Unaogopa nini?”
“Naona wanajeshi ni wengi?”
“Nipo katikati ya oparesheni, kuwa jarisi mke wangu sawa”
“Sawa baby, umebakisha umbali gani hadi kumfikia Stive?”
“Dakika kama mbili”
“Ok, kumbuka kwamba una mtu nyuma yako anaye kupenda na kuhakikisha kwamba kila jambo unalo lifanya linafanikiwa”
“Nimekuelewa mke wangu”
 
“Ninakupenda”
Nikashindwa kumjibu Hawa, baada ya kuwaona walinzi wawili wakija usawa wa eneo nililopo, taratibu nikatoa sime yangu ndefu na ni kali katika kila upande.
 “Dany……!!!”
Hawa aliendelea kunita, mwanajeshi mmoja akasimama pembeni ya mti huku akiwa na sigara mdomoni mwake, akatoa jogoo wake na kuanza kukojoa pembeni yangu kabisa huku mwenzake akimsibiria pembeni, kwa bahati mbaya mwanajeshi huyu akageuza kichwa sehemu nilipo, kabla hajafanya chochote, nikashusha sime yangu kwenye jogoo wake na kumtenganisha na mwili jambo lililo mfanya mwajeshi huyu kupiga ukelele mkali ulio nifanya niikate shingo yake na kuitenganisha kabisa na kiwili wili chake. Mwenzake akiwa anaweweseka kuishika bunduki yake sawa ili anishambulie, nikairusha sime yangu iliyo tua kifuani mwake na kumuangusha chini kama mzigo, nikamsogelea kwa haraka na kuichomoa sime yangu.
 
“Dany ni kutu gani kinacho endelea?”
“Kuna wajinga wawili nilikuwa ninawashuhulikia hapa”
“Imekuwaje?”
“Nimewasafirisha”
“Umewasafirisha!!!?”
“Yaa wanaimba mapambio huko mbinguni kwa sasa”
“Hhaaaa”
“Natakiwa kuondoka sasa”
Nikairudisha sime yangu sehemu nilipo itoa na kuzidi kusonga mbele huku mara kwa mara nikitazama simu hii kuangalia sehemu alipo Stive. Nikafani kufika chini ya kibanda ambacho kipo juu sana na juu yake wanakaa walinzi wenye bunduki pamoja na tochi kubwa ambayo wanaitumia kumulika maeneo ya chini. Nikifanikiwa kupita eneo hili, mbele yake ndipo kwenye geti ambalo ndipo alipo Stive na watu wake.
“Honey”   
“Bee”
“Nipo chini ya mnara wa ulinzi, nikipita hapa ndio ninafanikiwa kumpata Stive nini nifanye?”
“Hakuna njia nyingine ya kupita?”
“No hakuna, na ulinzi hapa ni mkali sana”
“Ngoja”
“Unataka kufanya nini?”
“Niangalie kamera za hapo”
“Hapa nilipo hakuna kamera yoyote”
 
“Dany”
“Yaa”
“Hakuna jinsi ya kupita hapo, ni lazima uwaue hao walinzi”
“Poa baby”
“Unaweza kufanya hivyo?”
“Why not”
“Good luck, na ninanatisha kamera inayo mulika ngazi hiyo”
“Sawa”   
Nikashusha pumzi taratibu, nikaanza kupandisha ngazi za kuelekea juu kwenye mnara huu. Nikapanda kwa tahadhari huku sime yangu nikiwa nayo mkononi mwangu, nikausukuma mlango wa kuingilia kwenye chumba chihi taratibu, nikawana wanajeshi wawili mmoja akiwa na kazi ya kuzungusha taa hii kubwa huku mwengine akiwa na kazi ya kutazama computer inanayo oyesha video za kamera zilizo tegwa eneo la karibu la hili eneo hadi getini. Kwa haraka nikaingia, na kuanza kuwashambulia wanajeshi hawa kwa kuwaua kikatili kwa kuwachinja shingo zao.
“Honey nimemaliza kazi”
“Safi songa mbele sasa”
“Mku tumekuta miili ya wanajeshi wawili wameuwawa kwa kuchinjwa, ninarudia tena nimekuta miili ya wanajeshi wawili imechinjwa kikatili. Ngome imevamiwa”
Nilisikia sauti ikitokea kwenye simu ya upepo iliyopo juu ya meza ndani ya hichi chumba, nikatazama kwenye computer nikamuona Stive na wanajeshi baadhi wakiondoka katika eneo getini na kukimbilia eneo ambalo niliwaua wanajeshi wa kwanza.


AISIIIII……….U KILL ME 119 


“Dany kuna nini kinacho endelea?”       
“Wameziona maiti za wanajeshi nilio wauoa”
“Mungu wangu, sasa itakuwaje?”
“Sina nafasi ya kumuua Stive kwa muda, inabidi nirudi tu”
“Kuwa makini mume wangu”
“Poa”       
Kwa hatadhari kubwa nikaanza kushuka kwenye mnara huu, huku bastola yangu moja nikiwa nimeishika mkononi mwangu, kutokana na kuweza kufahamu hii ngome kwa uzuri kabisa ikanilazimu kuanza kupita njia ambazo sio rahisi kwa wanajeshi kuweza kuniona.
“Dany upo wapi?”
“Nipo kwenye jengo la silaha hapa ndio nina rudi”
“Usije nyumbani kwa sasa”
“Kwa nini?”
“Walinzi wengi wamekuja huku nyumbani kwangu kuimarisha ulinzi”
 
“Si walinzi wako lakini?”
“Wapo walinzi wa Yudia, nina iamani wamekuja kwa makusudi zaidi”
“Ok nitajua nini cha kufanya”
Nilizungumza huku nikiwaona wanajeshi sita wakipita karibu yangu, nina imani wanamtafuta muuji aliye weza kuua wanajeshi walio waona. Uzuri wa sehemu niliyo jificha ni kwenye masanduku ya kuhifadhia silaha jambao sio rahisi kwa mtu kuweza kuniona. Wanajeshi hawa wakapita na eneo hili pasipo kuniona. Kichwa changu kiaanza kujawa na mawazo ya kufikiria ni sehemu gani ambayo ninaweza kwenda ili wanajeshi hawa wasiweze kuniona kabisa.
“Hawa”       
“Mmmm”
“Niambie kuna jambo gani linalo endelea?”
“Baba kuna kitu gani kinacho endelea”
“Kambi imevamiwa, inatubidi kuondoka na tutafute sehemu ambayo tunaweza kwenda”
Nilisikia mazungumzo kati ya Hawa na baba kupitia kinasa sauti ambacho Hawa amekivaa sikioni mwake na si rahisi sana kwa mtu kuweza kukiona.
 
“Baba tunakwenda wapi?”
“Sio muhimu kuweza kufahamu, jiandae tuondoke. Helicopter ipo tayari kwa ajili ya kutuchukua”
“Na ngome unamuachia nani?”
“Wapo watakao isimamia. Muandalieni nguo tuondoke”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwani Hawa ndio mtu pekee ambaye kusema kweli anafahamu uwepo wangu, katika eneo hili.
“Baba ninaomba unipe muda wa kufikiria hili”
“Hakuna muda wa kufikira hili, ngome imevamiwa, ni wakati wa kuondoka sawa”
Baba Hawa alizungumza kwa ukali sana.
“Baba niache nife kwenye hii ngome, sina kitu cha kupoteza ikiwa kila jambo kwenye maisha yangu uliweza kunipokonya. Nitakaa hapa na ni……..”
Nikasikia mlio wa kibao alicho pigwa Hawa shavuni mwake.
“Sihitaji kusikia ujinga kabisa. Mshikeni na mumpeleke kwenye helicopter”
“Sawa mkuu”
Nikaka kimya huku nikifikiria ni kitu gani ambacho ninatakiwa kukifanya. Kwa sehemu niliyopo ni karibu sana na kilipo kiwanja cha Helicopter, kwa haraka nikaanza kuelekea katike eneo hilo huku nikizidi kuwa makini kuhakikisha kwamba ninafanikiwa kuweka kufika katika kiwanja hicho.
“Hawa, Hawa”  
  
“Mmmmm”
“Ninakuja kwenye sehemu ilipo Helicopter”
“Mmmm”
“Nipo ninakuja mke wangu”
Nikazidi kuongeza mwendo kasi wa kuelekea katika eneo hilo la helicopter. Nikafanikiwa kufika kilipo kiwanja cha Helicopter, nikakuta wanajeshi zaidi ya kumi wakiwa na silaha, nikamuona Hawa akiwa ameshikiliwa na wanajeshi wawili wanao msindikaza. Sikuwa na jinsi za ya kuanza kufanya mashambulizi ya kuwaua hawa wanajeshi kila mmoja nikihakikisha ninamzawadia risasi yake itakayo msaidia kufika kuzimu pasipo yeye kutegemea. Hawa alipo ona ninaonyesha juhudi ya kuwashambulia wanajeshi wanao linda eneo hili, na yeye akaanza kuonyesha juhudi ya kupambana na wanajeshi walio mshika. Umoja wtetu ukaza matunda kwani wanajeshi wote ndani ya muda mfupi tuliweza kuwadhibiti.
Tukaingia kwenye helicopter, Hawa akaanza kuminya minya batani baadhi za hii Helicopter na taratibu ikaanza kuwaka.
“Unaweza kuendesha?”
 
Nilimuuliza Hawa huku nikimtazama
“Ndio”   
Tukaona wanajeshi wengi wakija kwa kasi sana, Hawa taartibu akaanza kuinyanyua Helicopter hii huku nikishangaa sana, kwani katika kipindi chote ambacho ninamfahamu sikujua kujua kama ni dereva mzuri wa kuendesha Halicopter.
Wanajeshi wakaanza kuishambulia Helicopter hii, ila tayari tulisha iacha ardhi na kuanza kuondoka katika eneo hili.
“Pole mume wangu”   
“Asante baby. Sasa hapa tunaelekea wapi?”
“Popote ili mradi tuwe katika eneo zuri, natambua baba atahitaji tufwatiliwe”
“Kwani ndani ya kambi kuna helicopter ngapi?”
“Zipo nne, mbili ni za kijeshi na hizi zilizo baki, ikiwemo hii ni helicopter za abiria wa kawaida”
Hawa aliendelea kuzungumza huku tukizidi kutokomea tusipo pajua. Mlio wa tahadhari ukaanza kulia kwenye hii helicopter.
 
“Nini hicho”
“Wanatufwatilia”
Hawa alizungumza huku akinionyesha kwenye kitivii kidogo chenye mshale unao zunguka wenye mwanga mwekundu. Nikaona Helicopter hizo jinsi zinavyo zidi kutusogelea kwa kasi kubwa, ubaya ni helicopter za kijeshi ambazo zinatumia kwenye mapigano ya anga. Hawa akaanza kuishusha Helicopter kwa kasi jambo lililo nifanya nimshangae.
“Una fanya nini?”
“Nahitaji pita usawa huu wa chini, nikiwa juu ni rahisi kwa wao kuweza kunishambulia, na hii ndio njia pekee ya sisi kuokoa”
“Unahisi kwamba helicopter zao haziwezi kuja usawa wetu”
“Sijafahamu kusema kweli ila tujaribu hii njia”
Usawa ambao Hawa anaipitisha hii Helicopter ni chini sana, jambo ambalo likaanza kunitisha kwani kosa lolote atakalo lifanya litapeleka sisi kuanguka, isitoshe eneo tulilopo lina miti michache sana iliyo achana sana. Milio ya risasi ikaanza kusikika nyuma yetu.
 
“Hawa ninakuomba ujisalimishe”
Tuliisikia sauti ya baba Hawa akizungumza kupitia earphone tulizo zivaa. Hawa akanitazama, akionekana kuwa na woga mwingi.
“Hawa ninarudia tena ninakuomba ujisalimishe”
“Baba siwezi kufanya hivyo”
“Nitaruhuhu marubani wangu wakuue”
“Acha nife, ila ninapigania penzi la mwanaume ambaye ninampenda kwenye maisha yangu”
“Ina maana upo na Dany?”
Hawa akaka kimya, nikamtazama ni nini anacho hitaji kukijibu.
“Hilo hupaswi kulifahamu baba”
Gafla helicopter yetu ikaanza kuyumba, hii ni baada ya kusikia kishindo kizito kikiipiga kwa nyuma.
“Dany ninakupenda, hata tukifa tambua kwamba ninakupenda”
“Ninakupenda pia mke wangu, niambie ni nini nifanye ili kuiokoa Helicopter?”
“Hakuna cha kufanya kwa maana imesha poteza muelekeo na tunaanguka chini”
 
Japo siku zote tunapambana ila hakuna kitu kibaya kama kifo ambacho mtu unaweza kukiona kwamba kinakwenda kutokea. Helicopter ikapiga chini kwenye ardhi na sote tukajikuta tukirusha na kujipigiza pigiza kwenye sehemu zilizopo karibu yetu.
Helicopter iaendelea kuserereka chini kwenye mchanga mwingi uliopo katika eneo hili. Kitu kikubwa ninacho muomba Mungu, atusaidie na helicopter hii isiweze kulipuka.
“Hawa, Hawa”
Nilimuita Hawa baada ya Helicopter kutulia na mchanga mwingi sana kuingia ndani ya helicopter kwa maana eneo tulilo angukia ni nusu jangwa.
“Hawa”
Hawa hakuitika zaidi ya kulala pembeni huku akionekana kupoteza fahamu. Nkajifungua mikanda ya siti niliyo kuwa nimejifunga, nikafungua mlango wa upande wangu na kutoka, japo nina majeraha machache kwenye mwili wangu ila sikuhitaji kupoteza muda. Kwa mbali nikasikia milio ya Helicopter ikikaribia kufika katika eneo tulilopo, nikafunga mlango wa upande wa Hawa, nikamtoa kwenye siti aliyo kalia huku akiwa anatokwa na damu kwenye paji la uso wake.
“Hawa, Hawa, Hawa”
Nilimuita huku nikimtingisha kwa nguvu, kidogo akanipa matumaini ya kufumbua macho yake.
 
Nikatazama eneo tulilopo, nikaona jiwe moja kubwa lenye tomba, nikamnyanyua Hawa na kuanza kukimbia naye hadi kwenye jiwe hilo, kitendo cha sisi kuingia nikaziona Helicopter za jeshi la baba Hawa zikizunguka katika eneo ambalo helicopter yetu imeanguka, nikatambua kabisa ni lazima wanaangalia kama sisi tupo hai au tumekufa.
“Dany”
“Ndio mke wangu”
“Upo salama”
“Ndio wewe je?”
“Kichwa honey kinaniuma”
“Ngoja tutatafuta jinsi ya kuondoka, ninaona wanamulika kuona kama tupo au laa”
Helicopter hizi zikaendelea kuzunguka kwa dakika tano eneo hili kisha zikaondoka, nikasubiria kwa muda kidogo kisha nikatoka nje ya jiwe hili. Kitu nilicho gundua kwa haraka kwamba wameshindwa kutuona ni kutokana na jiwe hili upande wa juu limefunikwa na mchanga na ni sehemu ya shimo ndio haijafunikwa na mchanga na imekuwa ni ngumu sana kwa marubuni wa helicopter hizo kutuona. Nikamtoa Hawa ndani ya shimo hili na kumsimamisha wima.
“Unaweza kutembea?”
“Yaa”
 
Nikatazama eneo hili vizuri nikaona kwa mbali kutoka hapa tulipo kuna eneo linalo waka taa. Tukaanza kutembea huku nikiwa nimemshika Hawa mkono, mwendo wetu haukuwa wa kawaida sana, ila nilihakikisha kwamba tunatembea mwendo utakao tuwezesha kuweza kufika katika eneo hilo linalo waka taa, na pana onekana kuna makazi ya watu.
“Eneo hili kama ninalifahamu”
Hawa alizungumza huku akitazama tazama kila sehemu ya eneo hili.
“Unalifahamu?”
“Ndio, twende”
Hawa akaanza kukimbia na mimi nikaanza kumfwata kwa nyuma. Tukaingia katika mji mdogo wenye nyumba za kawaida. Muda huu wa alfajiri watu wengi bado hawajaamka kutoka kwenye vitanda vyao. Tukazidi kukatiza kwenye nyumba za hili eneo, tukafika kwenye moja ya nyumba, Hawa akasimama na kutazama kila upande.
“Vipi?”
“Naangalia usalama”
“Kwani hapa ni kwa nani?”
“Kuna rafiki yangu mmoja anaishi hapa”
Hawa akaanza kugonga taratibu huku mimi nikiwa nimesimama pembeni huku nikiwa na bastola yangu mkononi.
 
“Nani?”
Nilisikia sauti ya kiume ikitokea ndani
“Mimi”
“Hawa?”
“Ndio”
Mtu huyo akafungua mlango, tukaingia kwa haraka, mwanaume huyu akanitazama kwa mshangao sana, nikamkazia macho.
“Ni mume wangu huyu, usiwe na shaka. Mkeo yupo wapi?”
“Chumbani, ngoja nikamuite”
Jamaa huyu mrefu kwenda juu na aliye jazia misuli ya mwili wake akandoka hapa sebleni, nikamsogelea Hawa na kulitazama jeraha lake lililopo kwenye paji la uso wake.
“Hujaumia sana”
“Wifi vipi?”
Nikageuka nyuma sikuamini macho yangu kumuona Mariam, ambaye naye baada ya kuniona akajikuta akistuka na kusima sehemu alipo, nikainyanyua bastola yangu kwa haraka na kumyooshea jambo lillilo mshangaza Hawa na mume wa Mariam.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...