Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 24, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 120 na 121 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA

Jamaa huyu mrefu kwenda juu na aliye jazia misuli ya mwili wake akandoka hapa sebleni, nikamsogelea Hawa na kulitazama jeraha lake lililopo kwenye paji la uso wake.
“Hujaumia sana”       
“Wifi vipi?”
Nikageuka nyuma sikuamini macho yangu kumuona Mariam, ambaye naye baada ya kuniona akajikuta akistuka na kusima sehemu alipo, nikainyanyua bastola yangu kwa haraka na kumyooshea jambo lillilo mshangaza Hawa na mume wa Mariam.
   
ENDELEA   
“Dany”       
Hawa aliniita huku akinishika mkono wangu ulio shika bastola, sikuhitaji kuushusha wala kuuteteresha, nilicho kifanya zaidi ni kukaza misuli yangu.
“Ulihisi kwamba sinto kukamata ehee?”   
Nilimuliza Mariam kwa hasira huku mikono yangu ikinitetemeka sana, jambo lililo zidi kuwashangaza Hawa na mume wa Mariam.
“Baby munajuana?”       
Mariam alimjibu mumewe kwa kutingisha kichwa tu kwamba ananifahamu, huku jasho jingi likianza kumwagika usoni mwake.
“Dany mume wangu mbona sielewi?”
“Hawa Mariam ndio muuaji wa familia yangu, ameiteketeza familia yangu kikatilia sana”
“Dany sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo, muulize Hawa atakueleza kila kitu”
 
Mariam alizungumza huku mwili ukizidi kumtetemeka hata matamshi yake yanatoka yakiwa yamejawa na utetemeshi mkubwa sana.
“Baby, ninakuomba utulie. Tupo katikati ya tatizo, ninakuomba utulie tafadhali”
Hawa alizungumza kwa sauti ya upole na laini, huku akiwa amenishika kifua changu, machozi ya hasira yakaanza kunimwagika huku nikiyang’ata meno yangu kwa hasira sana.
“Dany nakuomba sana tena sana ushushe silaha yako chini, kuna mambo mengi tunapaswa kuyazungumza”
Hawa aliendelea kuzungumza kwa upole sana akizidi kunisihi nimsamehe. Nikamtazama Mariam kuanzia chini hadi juu, nikashusha pumzi nyingi sana, kisha nikaushusha mkono wangu ulio shika bastola yangu.
“Tulia mume wangu kaa hapa”   
Hawa akanisogezea kiti, taratibi nikaka huku machozi yakinimwagika mfululizo, hasira ya mauaji yaliyo fanywa na Mariam kusema kweli inanisukuma kufanya mauaji yake ili maradi na mimi nijisikie amani japo kidogo katika moyo wangu. Nikamuona mume wa Mariam naye akishusha pumzi, akamshika mkono Mariam na kumkalisha kwenye sofa zilizopo hapa sebeleni.
“Hawa vipi asubuhi yote na majeraha usoni?”
“Ni hadisi ndefu kaka yangu, ila ngoja kwanza tulizungumze hili kati ya hawa watu wawili. Dany”
“Mmmmm”
 
“Nina tunaweza kuzungumza hili jambo?”
Nikanyanyuka kwenye kiti changu, nikachungulia dirishani, watu wote ndani ya seble macho yao wakawa wananitazama mimi. Nikazidi kukaa kimya huku nikisikilizia kwa umakini sauti ninazo zisikia kwa mbali sana zilizo nifanya niwe na wasiwasi mwingi.
“Dany”
“Shiii”
Nilizungumza huku nikimtulia Hawa kwa mkono, milio ya helicopter nilizo kuwa ninaisikia kwa mbali sasa nikaanza kuisikia kwa ukaribu kabisa, jambo lililo wafanya watu wote ndani ya seble kunyanyuka kwa haraka nak ukimbilia dirishani nilipo simama.
“Wanakuja”
“Kina nani Hawa?”
“Baba na watu wake wananitafuta na wanahitaji kuniua”
“Mungu wangu si wanaweza kukivamia kijiji hichi”
“Ndio maana yake, inabidi kutafuta njia ya kuondoka katika hichi kijiji”
 
Nilizungumza huku nikiishika bastola yangu vizuri.
“Kuna njia ya kutokea katika hichi kijiji”
Mariam alizungumza na kujikuta nikimtazama kwa jicho kali hadi akayakwepesha macho yake kwangu na kumtazama mume wake.
“Ndio kuna njia chini ya ardhi, tunaweza kuitumia na kuondoka kabisa katika hichi kijiji?”
“Basi hatuna muda wa kupoteza kaka yangu, niakuomba tuondoke”
“Basi ngoja tukavae haraka haraka”
Hawa na mumewe ambao wamevaa mavazi ya kulalia, wakaingia katika chumba chao na kutuacha sebleni.
“Una waamini?”
 
“Ndio nina waamini, ninamuoamini sana kaka yangu”
“Na imekuwaje Mariam akasema kwamba nikuulize wewe juu ya mauji ya wazazi wangu”
Kabla Hawa hajanijibu, nikaanza kusikia milipuko ya mabomu mita kadhaa kutoka hapa tulipo. Mariam na mumewe wakatoka chumbani wakiwa wanakimbia kila mmoja mkononi mwake ameshika mastola pamoja na tochi kubwa. Tukaingia kwenye moja ya stoo, wakatukabidhi mabegi ya mgongoni.
“Kuna nini humu?
Niliwauliza huku nikifungua begi langu, sikupokea jibu kwa mana nilicho kuuliza tayari nimesha kipatia jibu lake kwa maana kuna vibunda vya pesa za kimarekani, vilivyo pangwa vizuri na kujaa katika kila begi. Hawa akanikabidhi tochi yangu kubwa, kisha tukatoka humu katika chumba cha stoo. Tukaingia katika bafu hapo ndipo tukakuta mfuniko, mume wa Mariam akaufungua na akawa wa kwanza kuingia.
 
Akaingia Hawa, akafwatia Maria kisha nikamalizia mimi na kuufunga mfuniko huu ambao si rahisi kwa mtu kuweza kugundua kwamba kwa chini kuna njia, kila mmoja akawasha tochi yake na kuanza kumfwata mume wa Maria. Japo kuna nuka sana kutokana na haya maji machafu tunayo yakanyaga, ila hatuna namna zaidi ya kuzidi kusonga mbele kwani njia hii ndio itakuwa mkombozi wetu.
 
Kwa mara kadhaa Mariam aligeuka nyuma kunitazama, ila nikazidi kukazia macho.
“Tunatumia umbali gani kutokea huko yunapo kwenda?”
Hawa aliuliza huku tukizidi kutembea kwa mwendo wa kukimbia kidogo kidogo
“Ni umbali kidogo tujitahidi”
Tukafika sehemu tukakuta njia mbili  ambazo kila mmoja inaelekea upande wake, Mariam na mume wake wakatazamana.
“Nini?”
Niliwauliza huku nikiwa makini sana kwa maana siwaamini kabisa.
“Tunaangalia ni njia ipi nzuri ya haraka ambayo tunaweza kupita kutokea eneo ambalo lina usalama kabisa.”
“Kwa….”
Hawa akawahi kuniziba mdogo kwa maana hasira yangu anatambua kabisa kwamba bado haijaisha katika kumsamehe Mariam.
“Ongoza mwaya kaka yangu bora tufike”
“Twendeni huku”
 
Mume wa Mariam alizungumza na tukaanza kumfwata huku tukizidi kukimbia, tukatembea kwa masaa mawili na kujikuta tukitokea kwenye moja fukwe za bahari ambazo zimetulia na inavyo onekana kwamba hakuna dalili kabisa ya watu. Kila mmoja akajikuta akihemea kwa upande wake kwa maana ngija ngija tulizo kutana nazo huko tulipo toka kusema ukweli zimetushosha sana.
“Mungu ni mwema tumesalimika”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, akanisogelea na kunikumbatia huku kicha chake akiwa amekilaza kifuani mwangu.
“Ninakupenda sana Dany”
“Nina kupenda pia mke wangu”
“Jamani samahani”
Mume wa Maria alizungumza huku akitusogelea, taratibu tukaachiana na kumtazama ni kitu gani ambacho anahitaji kukizungumza.
“Itatubidi kukaa hapa kwa siku hii nzima, tukiacha mambo yakitulia basi tunaweza kubadilisha mfumo wa mazingira na kwenda sehemu nyingine mbali na hapa”
“Tuna chakula hadi tukae hapa?”
“Ndio tunacho, begi niliko kuwa nimelibeba mimi lina vyakula vilivyomo kwenye makopo”
“Sawa kaka yangu, hivi hapa hakuna watu?”
“Hapana fukwe hizi sio rahisi sana kwa watu kuweza kufika kwa manaa zimejificha sana na sio rahisi kugunduliwa”
“Wewe umezijuaje?”
 
Nilimuuliza mume wa Mariam huku nikimkazia macho, akamtazama Hawa kidogo kisha akazungumza.
“Nimejua mimi mwenyewe kutokana na utaalamu wangu wa kutengeneza njia zilizopo chini ya ardhi.”
“Kaka yangu nina shukuru ninakuomba ukazungumze na wifi yangu naona yupo mnyonge”
“Sawa dada”
Mume wa Mariam akaondoka katika eneo tulilo simama sisi.
“Dany muda mwengine ujaribu kuizuia hasira yako kuonekana wazi wazi”
“Siwezi kufanya hivyo ikiwa ninamuona adui yangu mbele yangu”
“Nalitambua sana hilo, ila ukweli ni kwamba Mariam hana makosa ya aina yoyote, yeye aliagizwa tu”
“Ataagizwaje kuua tena Watanzan wenzake?”
“Kumbuka Dany hata mimi mwenyewe nilikuagiza kwenda kumua Maria, pasipo kujau kwamba Mariam ni mtu mwema sana”
 
“Kwa nini unamtetea sana, au kifo juu ya wazazi wangu na wewe umehusika”
Nilizungumza kwa hasira na kumfanya Hawa kunitazama kwa macho ya mshangao, machozi taratibu yakaanza kumwagika, jambo lililo nifanya nijikute nikianza kuwa mpole.
“Am sorry mke wangu”
“Dany hivi laiti kama ningekuwa nimehusika na kifo cha wazazi wako leo hii mimi nisinge kuwepo hapa. Dany kuna mambo mengi sana ambayo huyajui na utanatakiwa kuyajua mume wangu”
Hawa alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi, nikamtazama Hawa nikamuona jinsi anavyo kumbatiwa na mume wake naye akionekana kulia sana kwa uchungu.
Nikamshika Mariam taratibu na kuelekea naye hadi pembeni ya maji ya bahari, tukavua mabegi tuliyo yaa migongoni na kuyaweka pembeni, nastola zetu nazo tukaziweka pembezoni maji. Taratibu tukaingia kwenye maji.
 
“Dany”
“Mmmm”
“Mwenzio sipendi kuogelea, nina ogopa”
“Twende tu usiogope”
Maji yakafika usawa wa viuno vyetu, taratibu nikamsogeza Hawa hadi kifuani mwangu, nikayashika mashavu yake kwa viganja vya mikono yangu, tukatazamana kwa sekunde kadhaa kisha tukaanza kunyonyana midomo yetu huki kila mmoja akiwa na hisia kakali. Hawa kwa haraka akaupelekea mkono wake wa kulia hadi kwenye zipu ya suruali yangu, akaifungua na kumtoa jogoo wangu. Akaanza kumchua taratibu.
“Dany nahitaji”
Hawa alizungumza huku akishusha pumzi nyingi na akionekana kuwa na hamu kubwa sana na mimi. Nikamshusha suruali yake, baada ya kuifungua mkanda, nilipo hakikisha kwamba nimeweza kukishika chake, nikamgeuza kwa haraka kisha nikamuinamisha taratibu.
Jogo wangu aliye cha Hawa.
“Dany taratibu nina umia”
“Shiii”
 
“Ninakupenda sana mume wangu”
“Ninakupenda pia Hawa wangu”
“Ninakuomba usiniache peke yangu Dany, nipo tayari kufa kwa ajili yako”
 
“Hata mimi pia mke wangu, nitakulinda hadi dakika ya mwisho katika maisha yangu”
Machozi ya furaha yakaanza kutumwagika kila mmoja. Tukatoka kwenye maji haya na kurudi nchi kavu na kuwakuta Hawa na mume wake wakiwa amekaa chini ya mti wa mkoko wakila chakula kila mmoja akiwa na kikopo chake cha chakula.
“Tumewaacha peke yenu”
“Hakuna tabu dada yangu”
“Wifi unaweza kuchukua chakula ndani ya begi”
“Hakuna tabu, shemeji yako atakuwa na njaa sana”
“Sio kivile ila nina njaa”
Hawa akanitolea kikopo chenye mchanganyiko wa chakula cha ubwabwa na maharage, nikakifungua na taratibu nikaanza kula huku nikimtazama Mariam kwa jicho la kuiba.
“Ehee dada ilikuwaje hadi useme kwamba baba anakuwinda?”
“Ni stori ndefu ndugu yangu, ila yote ni kutokana na shemeji yako hapa”
“Vipi baba hapendi mume wawili nini?”
“Yaa baba anahitaji kumuua shemeji yako ila kusema kweli sikupenda hilo jambo lijitokeze kwenye maisha yangu, kwa maana nina mpenda mume wangu sana”
“Shemeji pole kwa mikasa hiyo yote”
“Asante”
“Dany”
Mariam aliniita kwa sauti ya chini huku akinitazama usoni mwangu, sote tukakaa kimya huku tukimtazama.
 
“Natambua ya kwamba una nichukia, ila ninakuomba unisamehe sana kwa kila jambo ambalo limetoke kwenye maisha yako na mimi nikiwa ni chanzo wa kufanya hivyo”
Machozi yakaanza kumtoka Mariam usoni mwake.
“Niliamua kuachana na kila jambo baya kwenye maisha yangu, na kuamua kuishi kama mtu wa kawaida sana, roho yangu pia iliwindwa baada ya mimi kumaliza kuifanya kazi ya mauaji ya familia yako. Hawa wifi yangu yeye ndio aliye weza kunitafuta na kunieleza juu ya adhima ya mtu aliye nituma kuhakikisha kwamba ana niua na mimi ili kuendeleza siri hii isitoke”
“Nilimtafuta baada ya wewe kushindwa kumuua”
Hawa alizungumza na kunifanya nimtazame kwa mshangao.
“Hawa alinitorosha kunipeleka kwa kaka yake huyu hapa”
“Na mama yupo wapi?”
“Walimuua”
Moyo wangu ukajikuta ukizizima, kwa maana ninamfahamu vizuri mama Mariam ni mwanamke aliyeweza kunipenda na kuweza kunipa penzi lake japo kuwa alinipita umri mkubwa sana.
“Ni nani aliye muua mama yako?”
Mariam akaka kimya huku akinitazama, akamtazama Hawa ambaye naye pia alinitazama mimi kwa macho ya yaliyo jaa wasiwasi.
“Ni nani?”
“Ni baba yangu”
Hawa alizungumza kwa unyonge sana, nikajikuta nikiyang’ata meno yangu huku hasira dhidi ya maadui wangu wote ikizidi kuongezeka maradufu moyoni mwangu.
 
 AISIIIII……….U KILL ME 121  


Nikanyanyuka huku nikiwa nimekishika kikopo changu chenye chakula, wote wakanitazama, nikaanza kutembea kwenye fukwe hii, huku nizidi kuwa na hasira kubwa moyoni mwangu.
“Dany Dany”    
 
Hawa aliniita akiwa nyuma yangu, nikasimama na kugeuka.
“Dany natambua kwamba una hasira, ila….”
“Hawa ninakuomba unipe muda nahitaji kuwa peke yangu, sawa mke wangu”
“Sawa ila ninakuo…”
“Nimekuelewa mke wangu”
“Sawa, ngoja tukafirikirie kitu cha kufanya”
Hawa akaniacha na kurudi sehemu walipo kaa Mariam na mume wake. Nikatafuta moja ya jabali kubwa lililopo pembezoni mwa hii fukwe, nikakaa sehemu ambayo hakuna mtu yoyota anaweza kuniona. Nikatoa bastola zangu na kuziweka mbele yangu, nikatoa sime yangu nayo nikaiwake sehemu zilipo bastola. 

Taratibu nikapia magoti chini, nikainama na paji la uso wangu likahusa kwenye ardhi, machozi mengi yakaanza kunitoa huku maumivu makubwa yakiwa yamenitawala kwenye moyo wangu. Nikazidi kulia, kilioa ambacho kimekusanya maumivu ya matukio yote ya kuondokewa na wapendwa wangu hususani familia yangu. 

Nikamaliza zaidi ya nusu saa nikiwa nimeinama na kulia, nilipo hakikisha kwamba nimemaliza machungu yangu, nikanyanyua uso wangu, nikachukua sime yangu, nikajichana kidogo kwenye kiganja changu cha mkono wa kushoto, kisha damu yangu nikinyunyiza kwenye sehemu yalipo anguka machozi yangu mengi. Vishindo vya mtu aliye simama nyuma yangu nikajukua nikichukua bastola yangu na kugeuka kwa haraka. Nikamkuta Hawa akiwa amesimama, taratibu nikaishusha bastola yangu.
 
“Dany”   
Hawa alizungumza kwa mshangao huku akianza kunifwata akiwa na mshangao, akanishika mkono wangu wa kushoto na kuangalia damu zinazo endelea kunimwagika.
“Ohoo Dany umefanya nini mume wangu”
“Hakuna kitu”
Hawa kwa haraka akakata kipande cha shati lake, kisha akanifunga kwenye jeraha lililopo kwenye kiganja changu.
“Dany kwa nini unakuwa unafanya jambo kama hili”
“Leo ndio nimeomboleza vifo vya wale wote walio tangulia mbele ya haki, ila damu yangu haijamwagika bure, nitahakikisha kwamba walio wapelekea vifo vyao nilazima niwaue kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
“Usijali mume wangu hilo lote nitahakikiasha linakwenda kufanikiwa””
“Shukrani”
“Tumepanga mpango mmoja ambao utakuwa dhabiti katika kuianza hii kazi”
“Mpango gani?”
“Kuna yule mlinzi wangu naye amatoroka kwenye ngome, nimewasiliana naye, atakuja na boti kutuchukua hapa muda si mwingi”
 
“Isije kuwa ni mtego?”
“Ninamuamini sana haweza kufanya ujinga kama huo”
“Inabidi atakapo fika ni lazima sisi tujifiche”
“Kwa nini?”
“Kwa sasa mtu ninaye kuamini ni wewe tu na wewe ninakuomba uniamini mimi”
“Sawa mume wangu, nitakuamini hadi dakika ya mwisho ya maisha yangu”
“Sawa”
Hawa akaniokotea vitu vyangu nilivyo kuwa nimeviweka chini akanikabidhi, tukarudi sehemu walipo kaa Mariam na mume wake.
“Dada, Lusi amepiga simu anakuja muda si mrefu”
“Sawa”
“Lusi?”
“Ndio hiyo mlinzi wangu ninaye muamini sana”
“Sawa, cha kufanya nahitaji kila mmoja aweze kujificha, ili hata akifika katika hili eneo tuweze kuona kinacho endelea tusije kujikuta tunaingia kwenye mtego ambao utatuvurugia kila kitu”
“Sawa”
“Kitu kingine ambacho mumepanga baada ya kuondoka hapa?”
 
“Tumepanga tukateke meli moja ya abiria ambayo inabeba matajiri wengi wenye pesa, kupitia hiyo meli tutahakikisha kwamba tunapata pesa ya kutosha na tunaweza kuhimili zoezi lililopo mbele yetu”
Nikamtazama Hawa jinsi anavyo zungumza kwa kujiamini, nikajikuta nikishasha pumzi nyingi huku nikifikiria jambo la kufanya.
“Hiyo meli inatoka wapi na kuelekea wapi?”
“Hiyo meli ni ya Wamarekani, ila Lusi aliweza kuniambia kwamba itapita katika mkondo wa hapa Somalia”
“Mbona munataka tuingie kwenye bifu na nchi kubwa kama Marekani, wamarekani wanawathamini sana watu wao. Tukiwateka hapa watatufuta dunia nzima na wakitupata ndio basi tena”
“Dany hatuna la kufanya zaidi ya kufanya hivyo”
Mariam alizungumza huku akinitazama, kusema kweli, tunahitaji pesa, ilaha na uwezo wa kuweza kuendesha oparesheni yetu ya kuwaangamiza maadui zetu ila kwa hili ambalo wezangu wamelifanya wanataka kutengeneza uaduia na nchi kubwa duniani.
“Jamani moyo wangu katika hili kusema kweli umekuwa mzito”
 
Kwa mbali tukaona boti ikja usawa wetu kwa kasi, ikatubidi sote kutawanyika na kujificha kwenye miti hii ya mikoko kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake. Boti hii hiyo ambayo ni ndogo kiasi, ikasimama umbali kidogo na fukwe wa bahari. Akashuka Lisa na kuanza kuogelea hadi nje kabisa ya maji, akasimama na kuanza kuangalia kila upende. Hawa akajitokeza katika sehemu aliyo kuwa amejificha.
“Mkuu”
Lusi akamkimbilia Hawa na kukumbatiana naye, macho yangu yote nikayaelekeza kwenye boti, nilipo jihakikisha kwamba hakuna mtu yoyote kwenye boti, nikajitokeza na kuwafanya Mariam na mume wake kutoka katika maficho yao.
“Kambini kuna kitu gani kinacho endelea?”   
“Msako bado unaendelea, mzee kachafukwa baada ya kugundua kwamba ni kweli Dany alikuwa ndani ya ngome na yupo pamoja na wewe”
“Ila mawazo yao yapo vipi?”
“Wanajeshi wako wote wamewekwa chini ya ulinzi na wanahojiwa kwa mateso makali wakialezwa wataje ni sehemu gani ambayo wewe upo”
Nikamuona jinsi Hawa anavyo poteza amani, machozi yakaanza kumlenga lenga usoni mwake. 
 
“Jamani tuondokeni”
Nilizungumza, Lusi akanitazama kisha akamtazama Hawa.
“Sawa”
Hawa alizungumza kwa unyonge, tukaanza kuingia kwenye maji huku kila mmoja akwia ameshika begi lake ambalo alikuwa amelibeba. Hatukuchukua muda mwingi tukafika kwenye boti, sote kwa pamoja tukapanda na kuanza kuondoka eneo hili kwa kasi.
“Dany”   
“Inabidi kuhakikisha kwamba hii meli tunaiteka leo usiku”
“Hawa kitu tunacho kwenda kukifanya ni hatari sana”
“Ninajua ni hatari, tazama wanajeshi wangu, wakiumia kwa ajili ya hili lililo tokea, kama unanipenda ni vyema ukafanya hili kwa ajili yangu”
Hawa alizungumza huku machozi yakimwagika usonimwake, taratibu nikamkumbatia na kuanza kumbembeleza taratibu.
“Nitafanya kwa ajii yako”
“Kweli”
 
“Yaaa, Lusi amekuja na silaha za kutosha”
“Ngoja nimuulize”
Hawa alizungumza huku akiondoka katike aneo tulio simama na kuingia katika chumba kidogo alipo Lusi, nikasimama na huku nikangaia maji haya jinsi yanavyo kwenda.
“Dany”
“Naam”
Niliitika huku nikitazama pembeni, nikamuona Mariam akiwa amesimama kwa unyeyekevu, usoni mwake anaonekana ana kitu anacho hitaji kukizungumza kwangu.
“Vipi?”   
“Ahaa…ahaa natambua kwamba bado una chuki na mimi kwa sababu u……”
“Mariam hayo yote tulisha yazungumza, nimetambua kwamba umefanya kwa kufwata amri”
“Ni kweli”
Ukimya ukatawala kwa sekunde kadhaa huku tukiwa tumesimama sehemu ya mbele katika hili boti.
“Dany”
 
“Mmmm”
“Nikuulize swali?”
“Uliza?”
“Mahusiano yako ya sasa unayafurahia?”
Swali la Mariam likanifanya nimtazama kwa macho yaliyo jaa mshangao mkubwa, nikajikuta nikitabasamu.
“Kwa nini umeniuliza hivyo?”
“Hapana nijibu tu”
“Nisinge penda kuyaongelea sana hayo maswala ni vyema ukayapotezea kwa muda huu”
“Honey, amenieleza kwamba amekuja na silaha za kutosha. Ramani pia inayo onyesha jinsi tunavyo weza kuivamia hiyo meli ipo”
Hawa alizungumza sote tukabaki tukiwa tunamtazama. Ili kuficha kwamba hakuna kitu kinacho endelea kati yetu mimi na Mariam, akanigusa begani.
“Shemeji Mungu atakusaidia”
Mariam akaondoka na kumuacha Hawa akimsindikiza kwa macho.
 
“Alikuwa anahitaji nini?”
“Alikuwa ananiomba msamaha kwa mauaji ya wazazi wangu na nimemsamege kwa moyo mmoja”
“Jambo zuri mume wangu tusiishi kwa kinyongo ikiwa tunapango wa kufanya kazi moja”
“Kweli, twende tukaione hiyo ramani”
Nikaondoka na Hawa, tukaingia kwenye chumba alipo Lusi, akatukabidhi ramani hiyo huku yeye akiendelea kuendesha boti hii. Tukaanza kuifwatilia kwa umakini sana.
“Ila hii meli inaonyesha ina ulinzi mkali sana”
“Kwa nini?”
 
“Njia ambayo tunategemea sisi kuweza kupita ni kuzama kwenye maji na tunatakiwa kuingia kwenye meli hiyo pasipo wao kugundua, ila hata mafeni yake yaliyopo chini ndio yananipa mawazo sana”
“Mume wangu hilo lisikupe tabu, kwa maana kuna sehemu hii hapa japo ni ndogo na mtu ukikosea utajikuta mafeni hayo yakikukata ila inatubidi kufanya hivyo”
“Sawa mke wangu ila si kuna mitungi ile ya gesi ya oksijeni”
“Ndio vipo”
Tukazidi kusonga mbele, kwenye hii bahari ambayo mebele huoni unapo toka na Yuma huoni unapo tokea. Majira ya saa tatu usiku, Lusi akazima boti hii.
“Vipi?”
 
“Muda wa kwenda kuifanya kazi umewadia”
“Boti yenyewe ipo wapi?”
“Sasa hivi ni saa tau na dakika ishirini na nne, saa nne kamili meli itapita mita miambili kutoka hapa tulipo, kwa hiyo tutaogelea hadi kwenye meli hiyo, huu ni muda wa kila mtu kujiandaa”
Lusi alizungumza huku akimkabidhi kila mtu kifaa chake cha kuzamia kwenye maji, kila mtu akaanza kuvaa nguo hizi maalumu za kuegelea zenye miguu mipana ambayo inamsaidia mtu kuogelea rahisi akiwa chini ya maji. Nikavaa mtungi wa gesi mgongoni mwangu, kisha nikamvisha Hawa mtungi wa gesi mgongoni mwake, nikamfunga vizuri mikanda ya huu mtungi.
 
“Baby hii kazi tunayo kwenda kuifanya ni hatari, nikifa hakikisha kwamba kisasi unakilipiza kwa wale wote walio kutendea ubaya, hususani baba yangu”
Hawa alizungumza kwa sauti ya chini, taratibu akausogeza mdomo wake karibu na wangu, nikaupokea taratibu na tukaanza kunyonyana, nikamuona Mariam aliye simama nyuma Hawa, uso wake ukijikunja na moja kwa moja nikatambua kwamba wivu ndio unao mpelekea kuwa katika hali hiyo ya chuki na hasira.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )