Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 6, 2018

Chid Benz Aibukia kwa Diamond....Azungumza Maneno Mazito Kuhusu Madawa Ya Kulevya

Mwanamuziki wa kizazi kipya Chid benz ambaye alihusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya,jana aliweza kupewa nafasi ya kuongea katika sherehe za siku ya kuzaliwa ya msanii Diamond Platnumz na kuongea maneno ya kuumiza sana. 

Sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale  zilihudhuria na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali pia wadau mbali mbali wa sanaa ya muziki Tanzania. 

Chid benz alipata nafasi hiyo ya kuongea huku akipafomu nyimbo yake ya “Dar es salaam stand up” na kupokelewa kwa shangwe sana na wakazi wa kata hiyo ya Tandale waliohudhuria mahala hapo. 

Baada ya kumaliza kupafomu aliweza kumshukuru Diamond pamoja na wageni wote lakini pia shukrani nyingi alizirudisha kwa mashabiki wake na kuongea maneno yaliyomuumiza kila mmoja aliyefika mahala hapo kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya. 


“Madawa ya kulevya si mazuri lakini watu wanatumia na wanauza hii yote ni katika kutafuta hela, ila si kitu kizuri kama kinaweza kukusumbua ni vizuri kuachana nacho.

“Nashukuru kwa msaada wa Tale na Diamond kwangu, nashukuru sana kila kitu kiko sawa sasa cha msingi ni kufuatilia ili kupata maisha bora.

 

“Nashukuru kwa uongozi wa Wasafi kunipa nafasi, nafurahi kwa kila kitu kinachotokea hapa leo, kama wote tunakanyaga chini ya ardhi hakuna mtu anayeweza kupaa.” Alisema Chid Benz
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )