Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, October 5, 2018

Jiji la Mbeya Lashika Nafasi ya Mwisho Ukusanyaji Mapato

adv1
Jiji la Mbeya linalo ongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Mbunge wake, Joseph Mbilinyi maarufu kama “SUGU” limetajwa kuwa ni jiji la mwisho kwenye ukusanyaji wa mapato katika orodha ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam, Dodoma, Arusha, Tanga pamoja na mwanza.

Jiji lililo ongoza kwenye ukusanyaji wa mapato ni Dodoma ambalo lilitangazwa na Rais Magufuli mwaka huu, ambapo imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 25 ambayo ni sawa na asilimia 130 ya matarajio ya ukusanyaji kodi wa jiji hilo.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa halmashauri nchini juu ya hali ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri zao, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo ameilitaja Jiji la Mbeya lililo chini ya utawala wa CHADEMA limekuwa la mwisho kwa kukusanya bilioni 7.8 ambayo sawa na asilimia 70 ya matarajio.

“Naomba Wakuu wa Mikoa wanifuatilie ili wakafanyie kazi kwenye majiji yao, Jiji la Dodoma limekuwa la kwanza kati ya majiji sita kwa kukusanya zaidi shilingi bilioni 25 sawa na asilimia 130, wakati huohuo jiji la Mbeya limekuwa la mwisho kwa kukusanya bilioni 7.8 na makadiro yake yalikuwa bilioni 11”, amesema Waziri Jaffo.

“Kwa upande wa Manispaa, Iringa mjini ndiyo imeibuka kinara ikifuatiwa na Manispaa ya Temeke kwenye ukusanyaji wa mapato.” Ameongeza.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )