Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, October 25, 2018

Kigogo UWT Kortini Kwa Kugushi Cheti cha Ndoa

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Ester Kyara alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa  katika siku isiyojulikana jijini Dar, es Salaam, kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati wakati wakijua si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, alikana na ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya Sh 2milioni.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 21, mwaka huu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )