Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 4, 2018

Madiwani CHADEMA, CCM Wachapana Makonde Uchaguzi wa Naibu Meya Ilala

Katika hali isiyokuwa ya kawaida ngumi zilipigwa jana  Oktoba 3, 2018 kwenye ukumbi wa Anatoglo uliopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam ambako kulikuwa na  uchaguzi wa Naibu Meya.

Katika uchaguzi huo, Omar Kumbilamoto (CCM) alitangazwa msindi kwa kura 27 dhidi ya kura 25 za  Adam Rajabu (CUF) aliyepata kura 25 huku Mgombea Patrick Assenga (CHADEMA) akikosa kura hata 1.

Ngumi hizo zilimhusisha Diwani wa Tabata (Chadema) Patrick Assenga  aliyechapana makonde na baadhi ya madiwani wa CCM katika Ukumbi huo baada kuwepo kwa sintofahamu wakati wa kutangazwa matokeo  hayo ya uchaguzi huo

Ikumbukwe, Uchaguzi huo ulifanyika baada ya Kumbilamoto aliyekuwa naibu meya Ilala kwa tiketi ya CUF kujiuzulu na kuhamia CCM, akieleza ameshindwa kuwatumikia wananchi kutokana na chama chake kuwa na mgogoro wa uongozi.

Assenga alisema chanzo cha vurugu hizo ni baadhi ya kura kuharibika lakini mkurugenzi wa manispaa hiyo, Jumanne Shauri alipinga na kusema hakuna kura iliyoharibika.

“Mzozo ulianzia katika chumba cha majumuisho ya kura, nikiwa kama mwangalizi wa kura niliona baadhi ya kura zimeharibika na hazifai kwa mujibu wa uchaguzi, lakini Shauri na watu wengine walikataa.

“Niliamua kuzishikilia zile kura nne zilizoharibika baada kuona hivyo Shauri alitoka nje ya chumba na kuwaita polisi ambao walikuja kuninyang’anya zile kura na kunitoa nje ya chumba.”alisema Assenga.

Alisema baada ya kutolewa katika chumba hicho alikwenda kuzungumza na madiwani wenzake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ndipo wajumbe wa CCM walipomfuata na kuanza kurushiana maneno,  kisha kuanza kuchapana makonde.

Akizungumzia uchaguzi huo, mkurugenzi wa manispaa hiyo, Jumanne Shauri amesema ulikuwa wa haki na ulifuata taratibu zote na wajumbe walikuwa 52. CCM 26 na Ukawa kwa maana ya CUF na Chadema 26.

Amesema baada ya mchakato wa kuhesabu kura kukamilika, Kumbilamoto alipata kura 27 wakati Rajab  Penza wa CUF akipata 25.

Hata hivyo, Shauri amekiri vurugu kutokea akidai zilisababishwa na Assenga lakini polisi walifanikiwa kumdhibiti.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )